Zephania Ludigija ambaye ni Meneja wamauzo TIGO kanda ya Shinyanga na Tabora akiongea katika makabidhiano ya vitabu hivyo.
Dar es Salaam. Katika jitihada za kuendelea kuchangia elimu nchini, kampuni ya simu za mikononi ya Tigo imekabidhi vitabu kwa shule ya msingi Nyasa 1 (moja) iliyopo wilayani Nzega mkoani Tabora kupitia kampeni yake ya “Tigo tuChange”.

Shule ya msingi  Toangoma ya jijini DSM ndio iliyofungua mlango wa kampeni ya Tigo tuChange ambapo shule ya msingi Nyasa iliyopokea vitabu hivyo leo hii imekuwa ya pili na zoezi hili litaendelea kwa mikoa ya Singida, Kagera na Mtwara.

Zephania Ludigija ambaye ni Meneja wamauzo TIGO kanda ya Shinyanga na Tabora akimkabidhi vitabu Bi. Anne Mlimuka - Afisa mwandamizi ugawaji rasilimali TEA
 Akielezea madhumuni ya kampeni ya Tigo Tuchange wakati wa kukabidhi vitabu katika shule hiyo, Afisa mauzo wa mkoa wa Tigo Zephania Ludigija amesema Tigo ni sehemu ya jamii na kwa jamii yoyote ili iweze kuendelea elimu iliyobora ni nguzo muhimu na kwa kutambua hilo ndio maana tigo imeamua kuchangia elimu kupitia vitabu.

Kampeni hii ya Tigo tuChange inatokana na fedha zilizopatikana kupitia programu maalumu  iliyoandaliwa na Tigo tarehe 09 mwezi wa saba 2011 ambapo kuanzia saa tatu mpaka mpaka saa nne  mteja aliyenunua muda wa maongezi kuanzia shilingi mia tano na kuendelea fedha hiyo ilipeleckwa katika kampeni hiyo na jumla ya shilimgi  25,930,160 zilikusanywa ambazo ndizo zilizotumika kununulia vitabu.

Anne Mlimuka - Afisa mwandamizi ugawaji rasilimali TEA akiongea katika halfa hiyo ha kukabidhi vitabu.
 Ludigija ameongeza kuwa uzalendo wa watanzania na hasa katika kuipenda tigo umetoa msukumo wa wao kurudisha sehemu ya faida kwa jamii, ‘watanzania wameendelea kuwa msaada mkubwa kwetu na meendelea kutuunga mkono siku zote sasa na sisi kwanamna ya pekee hasa ukizingatia kuwa Tigo ni sehemu ya watanzania hatuna budi kurudisha sehemu ya kile tunachokipata kwa jamii inayotuunga mkono siku zote.’

Naye mkuu wa wilaya ya Nzega Florence Horombe amesema amefurahishwa sana na msaada huo ambao umeifikia shule inayoongoza kwa elimu wilayani kwake licha ya uhaba mkubwa wa vitabu unaoikabili na kuzitaka taasisi nyingine binafsi na za serikali kuchangia katika elimu na hasa kuiga mfano huu ambao kampuni ya simu za mkononi ya tigo imeuweka.
Wanafunzi wakinyoosha vitabu juu kuonyesha jinsi walivyofurahia.
 Akiongea kwa niaba ya Mamlaka ya elimu Tanzania TEA, ANNE MLINUKA amesema anafurahia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia sekta ya elimu. ‘Hatua hii ni nzuri na yenye manufaa kwa Taifa kwani vitabu vimeendelea kuwa tatizo kubwa katika sehemu mbalmbali ndani ya nchi na hivyo tunaishukuru tigo kwa kutufuata na kutaka ushiriki wetu katika kampeni hii na tungependa mashirika na taasisi binafsi na za serikali kuiga mfano huu wa Tigo katika kuchangia elimu ili tuweze kuhakikisha watoto wanapata nyezo muhimu za kujifunzia wakiwa shuleni”.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: