Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Askari Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, wameiomba Serikali kuangalia upya utaratibu wa matibabu kwa watuhumiwa wanaojeruhiwa ama kuugua wanapokuwa mikononi mwa Polisi ili waweze kutibiwa bure tofauti na ilivyo sasa ambapo mtuhumiwa anapopelekwa Hospitalini, askari hulazimika kumlipia matibabu wakati hapewi fungu.
Askari hao wametoa ombi hilo wakati wakizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Shamsi Vuai Nahodha, aliyopo kwenye ziara ya wiki moja katika mikoa ya Unguja kukagua majengo ya vituo vya Polisi na makazi ya Askari na kufanya mabaraza na askari kwa lengo la kujua matatizo na kero zinazowasibu.
Wamesema kuwa mara nyingi hulazimika kuwalipia watuhumiwa matibabu kutoka mifukoni mwao ama kurudi nao vituoni patipo matibabu kama aliyempeleka hakuwa na fedha mfukoni jambo ambalo wamesema ni hatari kwao na kashfa kwa Jeshi zima pale mtuhumiwa anapofariki akiwa katika kituo cha Polisi.
Askari hao wamesema kwa vile Askari Polisi na familia zao wanatumia kadi za bima ya Afya kwa matibabu yao, serikali iangalie uwezekano wa kubuni taratibu wa kuwa na kadi ya bima ya afya kwa kila kituo cha Polisi kwa ajili ya kusaidia matibabu kwa watuhumiwa.
Akijibu hoja hiyo, Mh. Nahodha amesema atalifuatilia suala hilo ili kupata ufumbuzi lakini anachojua ni kwamba jukumu la kuwatibu watuhumiwa ni la wizara ya Afya kwa vile Jeshi la Polisi halina mafungu kwa ajili ya matibabu kwa watuhumiwa.
Mh. Nahodha pia ametoa onyo kwa viongozi wa mamlaka za Viwanja vya Ndege na Bandari kutowazuia Askari Polisi kufanya kazi zao ipasavyo kwa visingizio vyovyote kwani pamoja na kuwa maeneo hayo yapo chini ya mamlaka husika, lakini Polisi ndiyo wenye wajubu mkubwa wa kuhakikisha Ulinzi na usalama katika maeneo hayo.
Amewataka viongozi wa maeneo hayo kutowa ushirikiano kwa Askari Polisi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama katika maeneo hayo ili kutekeleza majukumu yao kwa taifa pasipo kuwawekea mipaka lakini amesema ushirikiano huo ulenge katika kazi tu na sio katika njia za kujinufaisha binafsi.
Awali akitoa taarifa kwa Mh. Nahodha, kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa pamoja na Polisi kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa kiasi kikubwa, lakini mkoa huo unakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo la ufinyu wa bajeti usiokithi mahitaji yaliyopo kiusalama.
Naye Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema mpango wa Polisi Jamii ukishamiri utapunguza mlundikano wa kesi na watuhumiwa katika vituo vya Polisi na kwenye Magereza yetu kwani amesema uhalifu utadhibitiwa mapema mitaani kabla ya kufikishwa Polisi.
Kamishna Mussa amesema anaamini kuwa mpango wa Polisi Jamii ni ufumbuzi wa kukomesha uhalifu nchini na kwamba kama utapata msukumo ikiwa ni pamoja na wananchi kupewa elimu ya kutosha juu ya mpango huo, utaleta ufanisi katika mradi mpya wa Jeshi la Polisi wa utekelezaji wa Utii wa Sheria pasipo shuruti.

Toa Maoni Yako:
0 comments: