Kufuatia kupanda kwa Nishati ya Mkaa katika mji wa Sumbawanga, mkuu wa mkoa wa Rukwa Daniel Ole Njoolay ameingilia kati suala hilo na kusema tatizo hilo limetokana na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Kutozingatia mwongozo wa wizara ya maliasili na utalii na Divisheni ya misitu ambao unaelekeza kuwepo kwa uvunaji endelevu wa misitu katika maeneo yanayotegemewa .

Mkuu huyo wa mkoa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi yake, amechukua fursa hiyo kuomba radhi kufuatia hivi karibuni kupanda kwa nishati hiyo kutoka shilingi elfu nane kwa gunia hadi kufikia shilingi elfu hamsini.

Baada ya kukosekana kwa nishati hiyo ambayo iliwafanya baadhi ya kina mama kushindwa kufanya kazi zao za kila siku uku baadhi ya wafanyabiashara wakitumia fursa ya kununua mkaa huo uliokuwa ukiuzwa kwa mnada ili wauze bei ya juu.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Rukwa aliishutumu   halmshauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa kufanya Uzembe wa kutokaa vikao na kuomba radhi kwa wananchi.  

Njoolay ametoa wito kwa wafanyabiashaara watakaopatiwa vibali vya uvunaji wafuate taratibu za kufanya biashara ya mazao ya misitu ili kuepusha usumbufu uliotokea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: