Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Majeshi ya Ulinzi katika nchi za Afrika Mashariki yametakiwa kujenga uwezo wa kukabiliana na matishio mbalimbali yakiwemo ya uharamia wa kuteka meli za mizigo unaofanyika katika mwambao wa Pembe ya Afrika.

Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina amesema kuwa wito huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi,wakati wa kufunga zoezi la kijeshi lijulikanalo kama Natural Fire 11, lililokuwa likifanyika Zanzibar kwa kuyashirikisha majeshi ya ulinzi kutoka nchi nchi tano za Afrika ya mashiriki na Marekani.

Amesema utekaji na uporaji wa mali kutoka katika meli zinazofanya safari kwenye ukanda wa mwambao wa bahari ya Hindi umekuwa ukisababisha kupanda kwa bei za bidhaa kutokana na hofu ya wamiliki wa meli za mizigo kushindwa kupita katika maeneo yenye matishio.

Awali Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa hapa nchini, Dk.Husein Mwinyi, alisema lengo la zoezi hilo ni kukabiliana na matishio ya ugaidi, uharamia na kukabiliana na majanga mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa mafunzo hayo, Meja Jenerali Said Shaban Omar, amesema kuwa kupitia mafunzo hayo, majeshi hayo yamejenga uwezo na kupata mbinu mpya za kukabiliana na matishio mbalimbali kwa nchi wananchama.

Pamoja na wenyeji Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Majeshi mengine yaliyoshiriki katika mafunzo hayo ya pamoja ni ya kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Marekani.

Kabla ya kushuishwa kwa bendera za nchi washiriki, gadi za askari wa Majeshi hayo zilipita mbele na ya jukwaa kuu wakitoa heshima, kabla ya kushushwa kwa bendera za nchi shiriki kwa buruji maalumu.

Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Alfonso Leinhardt na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: