*Yaelekeza nguvu vijijini vya Tanzania

*Imezindua huduma za mawasiliano kanda ya ziwa kijiji cha  utegi  mara leo na nyanda za kusini nazo zimefikishiwa huduma

*Maeneo nane yamezinduliwa na kufikishiwa mawasiliano ndani ya wiki


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma bora za kuaminia na kwa bei nafuui ambayo inaoongoza kwa mtandao ulioenea zaidi nchini leo imeendelea kutimiza ahadi yake ya kufikisha mawasiliano vijijini.

Airtel imethibitisha kuwa mstari wambele zaidi ya mitandao mengine kwa kufikisha huduma za mawasiliano vijijini.

Akiongea kuhusiana na hili mwenyekiti wa kijiji bwana Jackson Ambilikile Kapoloso aliseme “tumefarijika kwa kufikishiwa huduma za mawasiliano hapa wilayani Rungwe wiki iliyopita.

Airtel ni mtandao peekee unaopatikana maeneo haya, ni waza na dhahiri uamuzi  umefanywa kwa wakati na  utasaidia wakazi wa Rungwe na vijiji vinavyoizunguka kukuza shughuli zao za kibiashara kwa urahisi, na wakazi wa hapa tuko tayari kuamia Airtel. Aliongeza Ambilikile.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “ ikiwa kati ya mipango ya kupanua na kuboresha mawasiliano nchini, hivi karibuni tumefikisha mawasiliano katika vijiji mbalimbali kwa kuzindua zaidi ya minara saba hapa mbeya.  Maeneo haya tuliyoyafikishia huduma wiki iliyopita yatatoa mawasiliano na huduma bora kwa wakazi wa hapa na vijiji vya jirani.

Tunajisikia fahari kuwaunganisha watanzania kwani tunaona ni jinsi gani mawasiliano yanavyoweza kuleta mabadiliko katika maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla, tunatambua Mawasiliano ni muhimu na si vinginevyo. Alingeza Mmbando.

Leo Airtel inazinduamawasiliano kanda ya ziwa kijiji cha utegi , huduma hizi hapa utegi zitawafikia pia wakazi wa vijji vy  Koaki, Ingili, Bukwe, Nyanduga,Otuna, Buturi, Yagoro, Kanguge, Mangra wilayani Rorya mkoani Mara. Huko ikiweka bayana mipango ya  Airtel katika kuendelea kupanua huduma zake ikitilia mkazo hasa katika kufikisha mawasiliano vijijini na kuhakikisha miji na vijiji nchini vinafikiwa.

Kadri tunavyopanua wigo wa mawasiliano ndivyo tunavyochangia katika kuongeza ubora wa maisha  kwa jamii na watu  na kuchangia katika maendeleo yaa nchi. Airtel tunafanya mawasiliano yaweze kufikiwa kwa urahisi nchini kote, sasa wakazi wa utegi na vijjiji jirani watapata huduma na bidhaa zetu, huduma hizi ni kama kupiga na kupokea simu, huduma ya internet, na promosheni mbalimbali. Huu ni wakati muafaka kwa  wakazi wa Ileje, Chunya, Tukuyu, Mwakareli, Rungwe, Mwanjelwa, Mbozi, Tunduma, Songwe, Uyole  na Mbalizi, Ku HAMIA Airtel sasa”  Alisisitiza Mmbando

Airtel inaendelea na Jitihada za kutanua mtando wake ikiwa ni kampuni yenye mtandao bora na wateja zaidi ya million sita na laki tano nchi nzima. Dhamira yetu na malengo ya kupanua mtandao wetu zaidi ni kuhakikisha tunatimiza lengo letu la uhuru wa kuongea ukiwa na Airtel.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: