Mwakilishi wa Uchina wa suala la amani ya Mashariki, Wu Sike, inapeleka ujumbe wa uongozi wa serikali ya Uchina ukithibitisha kuwa nchi hiyo iko tayari kuinga mkono mpango wa Palestina kuomba uanachama wa Umoja wa Mataifa.

Uthibitisho huo aliutoa kwa Katibu mkuu maalumu wa Raisi Bwana Tayyeb Abdul Rahim, katika makazi ya raisi huko Ramallah, jana.

Pia aliongeza kusema kuwa uongozi nchini mwake unafuatilia kwa karibu sana maendeleo ya mpango mzima na jinsi Palestina itakavyowakilisha suala lake hilo kwenye mkutano ujao wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu.

Alisema kuwa mpango huu kamwe hauendi kinyume na mpango wa kutafuata amani ya kudumu ya mgogoro na pia kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani kati ya pande mbili hizi, yaani Palestina kwa upande mmoja na Israeli kwa upande mwingine.

Ni wajibu wetu kuona kuwa taifa la Palestina huru linaanzishwa kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967, na Jerusalem ukiwa mji wake mkuu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: