Mratibu wa Maonyesho ya Sekta ya Magari, Ally Nchahanga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu Maonyesho makubwa ya Sekta ya Magari na utoaji huduma yaliyoandaliwa na Vision Investiments na yatajulikana kama 'The Tanzania Automotive Festival 2011' yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 7 hadi 9 mwaka huu katika viwanja vya Posta Kijitinyama. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Tulizo Chuzi, Mhadhiri wa Chuo hicho, Aziz Mdimi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Peter Garage, Peter Lyimo (wa pili kulia) na Mratibu Msaidizi wa Maonyesho hao, Dorice Malle.
Vision Investments inayo furaha kuwaletea kwa mara ya nne mfululizo maonyesho yanayo husiana na sekta ya magari na utoaji huduma “ Automotive Festival 2011” .
Maonyesho ya siku tatu ambayo yataleta pamoja wadau wanao husika na sekta nzima ya magari na huduma shirikishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 7 hadi 9 Oktoba 2011 na kiingilio kuwa ni 2,000/- wakubwa na watoto.
Maonyesho haya ya nne ni muendelezo wa maonyesho ambayo yalifanyika Oktoba Mwaka 2010. Na hii ni sehemu ya pekee ambayo inawapatia wafanya biashara, wapenzi na watumiaji wa magari na huduma shirikishi fursa yakukutana nakubadilishana ujuzi, mawazo na huduma juu ya sekta nzima ya magari.
Watoaji wa huduma za mikopo kama Benki ufundi na ushauri wa masuala ya magari watakuwepo.Wataalamu wa michezo ya magari nao watakuwepo kuonyesha ujuzi wao.
Kwa mujubu wa Mratibu wa Maonyesho hayo, Bw. Ally Nchahaga, “Tanzania Automotive Festival” Maonyesho haya hufanyika kila mwaka mwezi wa kumi.
Wananchi wategemee kuona na kujifunza masuala mbali mbali kuhusiana na sekta hii nyeti kwa uchumi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.Katika kuzingatia kuwa tuna sherehekea Miaka 50 ya Uhuru AutoFest haipo nyuma katika kuonyesha maeneo yakujivunia kama watanzania katika suala zima la usafirishaji na huduma zake shirikishi.
Kauli mbiu ya maonyesho haya ni “Defensive driving key to road safety”

Toa Maoni Yako:
0 comments: