Abiria zaidi ya 30 waliokuwa wakisafiri kwa basi la kampuni ya Sabco Ltd lenye namba za usajili T264 ATH kutoka wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuacha njia ya kupinduka katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.

Abiria wa ajali hiyo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com eneo la tukio kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 6 za mchana wakati basi hilo likijaribu kuyapita mabasi mawili likiwemo la Hood na New Force ambaye yalikuwa mbele na baada ya kuona lori mbele ndipo dereva alipoamua kulitoa basi hilo pembeni ya barabara na kupelekea kupasuka taili la mbele kulia.

Walisema abiria hao kisa Malila mkazi wa Kyela, Matina Mkinga mkazi wa Matema kyela Sarehe minga mkazi wa Ileje ,Elizabeth mkinga wa Ikombe Kyela na Bonifasi Daud mkazi wa Lumbila Ludewa kuwa bila jitihada za dereva uwezekano wa kupona ulikuwa mdogo zaidi.

Kwani walisema baada ya dereva kusikia mlio wa taili kupasuka hakuonyesha wasiwasi kwa kufunga breck na badala yake alitulia na kulitoa basi hilo taratibu nje ya barabara japo liliweza kuhama zaidi ya mita 10 kutoka nje ya barabara na kupinduka.

Dereva wa basi hilo Isaya maneno mkazi wa Ubungo jijini Dar amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni stelingi kuchomota na taili kupasuka.

Jeshi la polisi chini ya mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi limefika eneo la tukio la kutoa msaada kwa majeruhi hao.

Habari kwa hisani ya Francis Godwin
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: