Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, imetoa amri ya kusikitishwa kwa zoezi la kuwahamisha wakazi 1550 wa maeneo ya Kifaru, na Kibaga, kata ya Kinyerezi, manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam, mpaka manispaa ya Ilala itakaposhughulikia suala ya fidia kwa wananchi hao.

Jaji Augustino Shangwa alimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuacha kuwabugudhi wananchi hao katika maeneo yao na kuwaacha waendelee na shughuli zao za kila siku.

Amri ya jaji Shangwa inafuatia Court Injuction - (PINGAMIZI) ya manispaa ya Ilala mahakamani hapo la kuitaka mahakama kuu isiyasikilize maombi ya wakazi hao waliyoyawasilisha mahakamani hapo kuiomba mahakama kuu itoe amri ya kuizuia manspaa ya Ilala kuwahamisha katika maeneo yao.

Awali, Wakili wa serikali katika kesi hiyo, John Wanga alipinga amri ya mahakama ya kuitaka manispaa ya Ilala iache kuwabugudhi wananchi hao kwa kuwataka wahame katika makazi yao akieleza kwamba maombi ya wakazi hao ni batili kwani hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi yao mahakamani hapo, na ndipo Jaji Shwangwa akaeleza kwamba mahakama aina haki ya kuwasaidia wananchi hao wa kutoa amri ya kutobughudhiwa zaidi.

Jaji SHANGWA amewataka wakazi hao kupitia kwa wakili wao, MATHIS OMARI KISEJU, kuwasilisha majina kamili ya wawakilishi wao katika kesi hiyo na orodha ya wahusika kesho kutwa na kwamba kesi hiyo itatajwa tena mahakamani Julai 15, 2011.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: