Waziri wa mambo ya ndani, Shamsi Vuai Nahodha amefungua mkutano wa wamiliki na viongozi wa vyama vya abiria, wenye lengo la kujadili kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa ufuatiliaji wa mabasi yaendayo mikoani, wa CAR TRACK SYSTEMS.

Sambamba na hatua hiyo, Waziri Nahodha amewataka wamiliki na viongozi wa vyama vya Madereva, kushirikiana na serikali katika kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani, ambazo zimekuwa zikisababisha wananchi wengi kupoteza maisha yao, na wengine wakiachwa majeruhi kutokana na ajali hizo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: