Na Andrew Chale, Zanzibar
Mwanamuziki wa kimataifa wa ragga na mshindi wa tuzo za Grammy 2011, Orville Richard ‘Shaggy’ kesho anatarajia kupanda jukwaani ndani ya Ngome kongwe ukumbi wa Mambo kutumbuiza shoo kali huku akisindizwa na wanamuziki nyota wa hapa nchini sambamba na kundi la THT Dancers.
Kwa mujibu wa Meneja masoko na mmoja wa waratibu wa Tamasha la Filamu za Nchi za majahazi maalufu ZIFF, Laurian Kipeja alisema kuwa, mwanamuziki huyo wa kimataifa atapanda jukwaani hiyo kesho majira ya usiku na kupiga shoo kali nay a aina yake huku akisindikizwa na wasanii mahiri wa hapa nchini.
Kipeja alisema kuwa, tayari tiketi za shoo hiyo zimeanza kutolewa katika ofisi zilizopo makao makuu ya ZIFF ndani ya Ngome kongwe huku bei zikiwa nafuu kwa kila mmoja.
“Shoo hii itakuwa ni ya pekee nay a aina yake kwa wakzi wa Zanzibar na wageni mbalimbali huku kima cha juu kwa V.I.P. ni laki moja (100000) na (50,000) na vya kawaida kwa wageni ni 30,000 huku wazawa ama wakazi ni 15,000” alisema Laurian.
Aidha, inadaiwa Shaggy atatua visiwani hapa na boti maalum loe na kasha saa sita mchana atafanya mkutrano na vyombo vya habari sambamba na kufunga vyombo. Mpaka sasa mwanamuziki huyo ambaye kihistoria ni mwanajeshi na aliyeanza muziki wake huo lipokuwa vitani, natamaba na vibao vya Boombast, Angel, Sex lady, Feel the Rush na vingine vingi sambamaba na kuimbva kwa staili mbalimbali awapo jukwaani.
Kwa upande wake, meneja wa ZIFF, Danny Nyalusi alisema wasanii watakao msindikiza Shaggy ni pamoja na Sultan King, na kundi la THT ambapo watapiga shoo kali ambayo haijawai kutoea visiwani humo.
Pia alisema kuwa kwa mwaka huu, kaulimbiu ya ZIFF imebeba ujumbe wa ‘A season of Visions’ na kwa mara ya kwanza, tamasha hilo li,ezaminiwa na mdhamini mkuui Kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kinywaji chake cha Tusker Malt, Prime Time promotion, Coconut FM, Azam Marine Co ltd, TTB, Common Wealth Foundation, Coca-Cola, GIZ (TZ), na Ujerumani, Smole, Movenpick, Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa.

Toa Maoni Yako:
0 comments: