Mshindi wa shindano la Serengeti Fiesta Freestyle Raymond Shabani kutoka mjini Mbeya akimwaga salamu zake kwa mashabiki. Katika shindano hilo Lotas kutoka mkoani Morogoro ameweza kunyakua nafasi ya pili.Mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 Dj Fetty ambaye pia alikuwa ni mratibu wa shindano hilo la Sererengeti Fiesta Freestyle 2011 akimtangaza mshindi ambaye ni Raymond Shabani kutoka mjini Mbeya katika fainali za shindano hilo.Mashabiki waliohudhuria katika fainali za shindano la Serengeti Fiesta Freestyle 2011, Coco Beach jijini Dar es Salaam.Mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 jijini Dar Ruben Ndege ambaye pia ni mc wa shindano hilo wakijaribu kuongea na majaji na mashabiki waliohudhuria shindano hilo. Kushoto ni mshiriki kutoka mkoani Mbeya, Raymond Shabani pamoja na mshiriki mwenzake Lotas kutoka mkoani Morogoro. Mshiriki kutoka mkoani Mbeya, Raymond Shabani akionyesha umahili wake wa kuchana mistali mbele ya mshiriki mwenzake Lotus kutoka mkoani Morogoro katika fainali ya shindano la Serengeti Fiesta Freestyle iliyofanyika Coco Beach jijini Dar es Salaam. Katikati ni mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 jijini Dar Ruben Ndege ambaye pia ni mc wa shindano hilo wakifuatilia kwa makini.Majaji wa shindano la Serengeti Freestyle 2011 kulia ni msanii wa hip hop nchini Fid Q akiwa pamoja mkongwe wa muziki huo wa hip hop Zavara wakifuatilia kwa makini zoezi la kumtafuta mkali wa kuchana ambapo ilikuwa ni fainali ya mashindano hayo yaliyokutanisha mikoa ya mitano ambayo ni Mbeya, Arusha, Mwanza, Morogoro na Zanzibar.
Home
Unlabelled
RAYMOND SHABAN KUTOKA JIJINI MBEYA ANYAUA TAJI LA SERENGETI FIESTA FREESTYLE 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments: