Naibu Mkurugenzi Mkuu akifunga mafunzo ya siku tatu ya huduma kwa mteja kwa watumishi wa idara ya uanachama yaliyokuwa yakiendelea mkoani Morogoro katika ukumbi wa Amabilis, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa NHIF Bwn. Deusdedit Rutazaa na kushoto kwake ni meneja wa kanda ya ziwa wa mfuko huo Bi Imelda Likoko.

Wakipeana miongozo namna ya kusimamia na utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya mfuko wa taifa wa Bima ya Afya wakati wa mafunzo ya huduma kwa mteja kwa watumishi wa idara ya uanachama hususani uboreshaji wa huduma kwa wanachama kulia ni mkurugenzi wa operesheni wa NHIF Bwn.Eugen Mingongoti kushoto ni meneja wa uanachama wa NHIF Bi Ellentrude Mbogoro.

Wakifuatilia kwa makini watumishi wa idara ya uanachama hotuba ya mgeni rasmi wakati wa hitimisho wa mafunzo elekezi ya siku tatu ya huduma kwa mteja ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi mkuu wa NHIF Bwn. Hamis Mdee, amewataka utekelezaji wake uwe wa vitendo kupitia mafunzo waliyoyapata hili kufanya mrejesho stahiki wa huduma bora kwa wadau na wanachama wa NHIF. Mafunzo hayo yalifungwa jana mjini Morogoro.

PICHA NA MDAU PAUL MARENGA-NHIF MORO

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: