Bila ya shaka utakuwa umeshawahi kuona katika baadhi ya filamu, mwanaume wa makamo akishiriki tendo la ndoa na mwanamke mrembo halafu ghafla anapofika kileleni bwana yule macho yanamtoka pima!, anashindwa kupumua, anashindwa hata kutoa sauti ya kuomba maji - amepata mshtuko wa moyo, anakufa. Je, tendo la ndoa ni hatari kwa wanaume wanaolishiriki?
Kuna tafiti zinazoonesha kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba tendo la ndo linawamaliza wanaume wanaolishiriki kwa kuwasababishi mshtuko wa moyo, lakini pia utafiti mpya uliofanya na taasis ya Havard Men's Health Watch unasema uhusiano huo sio mkubwa kama ilivyokuwa ikidhaniwa awali.
Utafiti huo unasema kuna uwezekano kuwa katika vifo 200 vya mshtuko wa moyo labda ni kimoja tu ndio utasikia kimetokana na mchezo huu ulitukuka.
"Kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka 50 na zaidi uwezekano wa kukumbwa na mshtuko wa moyo wakati wowote ule moja kati ya milioni," anaandika Daktari Harvey B. Simon, mhariri wa jarida la kitabibu katika chuo kikuu cha Havard. "Ni kweli kwamba tendo la ngono linaongeza uwezekano wa mwanaume kupigwa shoti ya moyo kwa kama mara mbili katika milioni. Na kwa wanaume ambao tayari wanayo matatizo ya moyo uwezekano wao wa kuaga dunia mara tu wanapofika kileleni ni 20 katika milioni."
Utafiti huu mpya unaonesha kwamba ni vyema wanaume kufanya ngono zaidi kwani inasaidi kuupa moyo mazoezi tofauti na wale ambao wanakaa muda mrefu bila kupiga gemu.
Utafiti wa taasis moja ya huko Massachusetts, Marekani, umeonesha kwamba wanaume wanaweza kupitisha mwezi bila kupiga gemu wanayo nafasi kubwa ya kujitengenezea matatizo ya moyo, kwani misuli ya mioyo yao inakuwa dhaifu tofauti na wale wanaopiga gemu mara mbili kwa wiki.
Dr. Simon anasema tendo la ndoa ni zoezi zuri sana kwa afya ya misuli ya moyo na amelilinganisha zoezi hilo sawa na zoezi la kucheza mpira wa meza (table tennis) au kufanya usafi katika bustani.
Dr. Debby Herbenick, mtaalamu na mkufunzi wa masuala ya ngono, ambaye pia ameandika kitabu cha "Because It Feels Good" anasema, "Ni jambo la kufurahisha kwamba ngono sio sababu kubwa ya watu kupata mshtuko wa moyo mara wanapokaribia kileleni, kama ingekuwa hivyo basi wanaume wengi ambao wana matatizo ya moyo tayari wangeogopa kujihusisha na tendo hilo takatifu."
Hata hivyo wataalamu hawa wawili wanashauri mtu ambaye amaeshawahi kukutwa na mshtuko wa moyo ni vyema akawasiliana na daktari wake kwanza, kwa maelekezo zaidi ya namna ya kuandaa mechi yako. Wanashauri pia wanaume wa aina hii kutotumia dawa za kuongeza nguvu kama Viagra, au supu ya pweza, na mkuyati.
Wanasema kipimo kizuri cha kukuonesha kama uko fiti kwa ajili ya mechi ni kujaribu kupanda ngazi za ghorofa, na kama unafika juu ukiwa unahema kupindukia inabidi kuwa makini na mechi yako, kuna hatari unaweza kutolewa katika mashindano na hata kuzikwa.
Mwisho kabisa wanashauri kwamba kama una matatizo ya moyo ni vyema ukapiga gemu na mtu ambaye mnafahamiana vyema na mlishawahi kupiga gemu awali. Hii ni kwa sababu mwenzi wako atakuwa na uelewa mzuri wa spidi gani akupeleke nayo, asije akakupeleka kwenye Highways wakati wewe ni mtu wa barabara za uchochoroni tu.
Wanaume mpo? Hili ni fundisho zuri pia kwa wale kina dada ambao wameamua kukamata vibabu, muwe na simile kwa wenzi wenu msije wekwa eda mapema.

Toa Maoni Yako:
0 comments: