ASKARI wa Israeli walimtia mbaroni jamaa mmoja wa Kipalestina aitwaye Ahmed Ali Mahmoud, miaka 36, katika eneo la Shaare Zedek, magharibi mwa mji wa Jerusalem jana, licha ya majeraha aliyoyapata kutokana na kipigo kutoka kwa askari hao.

Matukio hayo yalitokea huko Al-Issawiya, kitongoji kimojawapo kilichoko jijini Jerusalem.

Jamaa zake walisema hali yake siyo mbaya sana, licha ya kupigwa risasi mguuni mwake.

Hivi sasa anauguza majeraha ya risasi mguuni mwake na usoni, lakini Askari wa Israeli wanaendelea kumshikia huku kafungwa pingu mikononi na miguuni mwake.

Wanasema Mahmoud alipigwa baada ya askari hao wa Israeli kuvamia kijiji cha Al-Issawiya ambapo askari hao, bila huruma wala kujali utu na ubinadamu, walimtia mbaroni mpwa wake, kijana wa miaka tu. Alizimia baadaye kutokana na kuvuja damu nyingi, ndipo alipopelekwa hospitalini.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: