Mr. II au wengune walimjua kwa jina la Sugu akiwa na Mrisho wa Global Publisher...hivi sasa Mr. II ametimiza miaka 15 ndani ya muziki wa Bongo, anakuwa msanii mkongwe wa Hip Hop ya Bongo kuliko wengine waliyopo sasa!

-------------------------
The very strong sterling ndani ya Bongo Flava industry, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Mr. II’ yupo hewani kwa mara nyingine na sasa anakuja na mawe 10 yaliyosimama kama madini ya dhahabu ndani ya albamu yake ya 10 inayosimama kwa jina la Veto.

Mr. II a.k.a Sugu ataitambulisha albamu hiyo Desemba 24, 2009 (Mkesha wa Krismasi), katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Mzigo kamili umeandaliwa nchini Marekani, kwenye Studio ya S&S Records iliyopo Brooklyn chini ya maprodyuza, Stiggo na Puzo.

Stigo ‘amefanza’ mawe saba na Puzo amegonga mawili, huku wana-Hip Hop wenye heshima Bongland kama Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, John Simon ‘Johmakini’ na Ahmed Dolla ‘Balozi’ kwa pamoja wameingiza vocal kwenye albamu hiyo.

Wamarekani wawili, Andre ambaye ni mchizi pamoja na mwanadada Shanice, wameingiza sauti na kukamilisha ujio mpya wa Sugu ambaye tangu mwaka 1994, kila akitoka mandhari ya Bongo hubadilika kutokana na vishindo vyake.

Moto wa Diamond Mkesha wa Krismasi, utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 15 (15th Anniversary) ya Sugu ndani ya game ya Bongo Flava, kwani tangu mwaka 1994, bado ametuama pale pale on top.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: