Kampuni ya kutengeneza vinywaji baridi ya Cocacola kanda ya ziwa imeendesha matibabu ya bure ya macho na magonjwa mengine kwa watu wenye umri mkubwa wilayani hapa.
Cocacola ikishirikiana na klabu ya Lions ya mjini Mwanza imeanzisha matibabu hayo mjini hapa kwa wazee kutokana na kundi hilo kusahaulika na jamii kwa sababu mashirika ya kiserikali na yale ya binafsi yamekuwa yakijikita zaidi katika makundi maalum ya watoto,wanawake na waathirika wa virusi vya ukimwi.
Akifungua matibabu hayo katika hoteli ya CMG mjini hapa leo,mkurugenzi wa Cocacola kanda ya ziwa Christopher Gachuma amesema kampuni hiyo iliamua kutafuta wadau wengine wa kuhudumia jamii kusaidia watu wenye umri mkubwa kutokana na kundi hilo kusahaulika zaidi katika mipango ya kuwahudumia hususan kitabibu.
Amesema kampuni yake zaidi ya kutafuta ufanisi wa kibiashara zaidi wamejikita katika kurudisha huduma kwa jamii na kuhakikisha kundi hilo la wazee wanapata maisha bora kwa kuwa katika umri huo wengi hupoteza uwezo wa kujihudumia
Bw.Gachuma ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM amesema baadhi ya wazee waliokuwa watumishi wa serikali na umma wanapostaafu kazi zao wanashindwa kujikimu na kiiinua mgongo kiduchu wanachopewa ambacho hakikidhi mahitaji kutokana na kupanda gharama za maisha siku hadi siku.
Kwa upande wake Meneja wa mauzo na usambazaji wa CocaCola kanda ya ziwa Phillip Gucha alisema kwa siku ya pili mfululizo wameweza kuhudumia wagonjwa 700 wenye umri mkubwa kutoka vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo na matibabu hayo yameshirikisha wataalam wa afya kutoka hospitali ya wilaya ya Tarime ambapo pia matibabu ya magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na malaria yametolewa.
Naye mwenyekiti wa klabu ya Lions ya mjini Mwanza Patel Shirish alisema mpango huo ni moja ya mikakati ya taasisi hiyo kuhudumia jamii ambapo pia katika kanda ya ziwa wameweza kutoa misaada mbalimbali kwa watu wasiobahatika katika jamii.
Amesema klabu hiyo yenye matawi 30 nchi nzima mbali na kuendesha matibabu ya bure wanatoa huduma katika jamii ikiwa ni pamoja na kuwapatia maji salama kwa kuchimba visima na kufadhili watoto wasiojiweza kuendelea kielimu kwa kuwalipia karo mbalimbali kila mwaka.
Huduma hiyo inafikia kilele kesho ambapo mkuu wa wilaya ya Tarime Frank Uhahula anategemewa kufunga matibabu hayo ambapo waandaaji hao wamesema yatafikia zaidi ya wagonjwa 1000.

Toa Maoni Yako:
0 comments: