Sefora Messele Ghebreezga biheir
Date of Birth: 19-09-1991 Height 180
Hobbes: swimming, reading
Selamawit Zerabruck Ghebreslassie
Date of Birth: 19-08-1991 Height 172
Hobbes: reading, Traveling,

Eritrea imekuwa nchi ya kwanza kutangaza warembo wake katika mashindano ya kimataifa ya urwembo ya Miss East Africa mwaka huu yatayofanyika December 18, 2009 jijini Dar. Warembo hao walipatikana katika mashindano ya kuvutia ya urembo yaliyofanyika jijini Asmara Nchini humo hivi karibuni.

Warembo watakaoiwakilisha Eritrea katika mashindano ya mwaka huu niSelamawit Zerabruck Ghebreslassie na Mesele Ghebreezgabiheir.Mwaka jana Nchi ya Eritrea pia ilikuwa ya kwanza kutangaza wawakilishi wake katika mashindano ya Miss East Africa 2008 yaliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ambapo iliwakilishwa na warembo Rahwa Ghebrehiwet pamoja ya Menal Hussien ambapo Rahwa Ghebrehiwet alifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu.Mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa huandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar.

Nchi 14 za ukanda wa Afrika mashariki tayari zimeshathibitisha kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ambazo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, zingine ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, visiwa vya Seychelles, Re union, Madagascar, Comoros na Mauritius.

Wakati huohuo ile bahati nasibu ya Miss East Africa ya kuchangia yatima ambapo mshindi wa kwanza atajishindia gari jipya aina ya Range Rover sport inaendelea na watu wote wameombwa kushiriki bahati nasibu hiyo.

“Tunawaomba watu wote washiriki kwa kuandika neno SHINDA kwa kutumia simu zao za mkononi na kutuma kwa sms kwenda namba 15567 ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali na wakati huohuo wakichangia yatima wa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla”
Imeandaliwa na kusainiwa na Rena Callist, CHAIRMAN, MISS EAST AFRICA BEAUTY PAGEANT.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: