Wafanyabiashara wawekezaji mkoani Rukwa wameipa changamoto serikali ya mkoa huo kuimarisha mazingira ya uwekezaji ili kuharakisha kasi ya maendeleo ya kiuchumi ya mkoa huo.

Taarifa ya kampuni moja ya uwekezaji ktk sekta ya elimu ya Saint Aggry ya mkoani Mbeya imeelezea jinsi ukosefu wa maji umeme na huduma nyingine kwenye maeneo ya uwekezaji unavyopunguza kasi ya kuwekeza mkoani Rukwa.

Akisoma taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Rukwa bw Daniel Ole Njoolah wakati wa kuweka jiwe la msingi la shule ya sekondari ya kidato cha kwanza hadi cha sita mkurugenzi bw Mboka.

Mwambusi ameeleza kuwa miundombinu duni inaongeza gharama za uwekezajiAkijibu taarifa hiyo mkuu wa mkoa wa Rukwa amekiri kuwapo kwa upungufu wa miundombinu imara hali inayochangia kasi ndogo ya wawekezaji kuja mkoani humo licha ya juhudi za kuutangaza mkoa huo kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji.

Ameeleza kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo halmashauri za wilaya mkoani humo zimeelekezwa kuweka mapema mahitaji muhimu ktk maeneo ya uwekazaji ili kurahisisha uanzishaji wa miradi ktk eneo husika
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: