IMETOLEWA NA MH. DR. BATILDA BURIAN (MB), WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA) KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA HIFADHI YA TABAKA LA UKANDA WA HEWA YA OZONI TAREHE 16 SEPTEMBA, 2008
Ndugu Wanahabari,
1. Chimbuko
Kama mnavyofahamu kila tarehe 16 Septemba Jumuiya ya Kimataifa huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa 49 wa tarehe 19 Desemba 1994 katika azimio nambari 49/114. Maadhimisho haya ni kumbukumbu ya kupitishwa kwa Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol), mwaka 1987 huko Montreal Canada. Mkataba wa Montreal unahusu kemikali zinazosababisha kumong’onyoka kwa Tabaka la Ozoni. Tanzania imeridhia Mkataba wa Montreal pamoja na marekebisho yake; hadi sasa nchi 193 zimeridhia.
Ozoni ni hewa mithili ya oksijeni iliyoko kwenye anga hewa ya juu, umbali wa takriban kilometa 10 hadi 50 juu ya sura ya Dunia. Kazi yake kubwa ni kuchuja sehemu kubwa ya mionzi ya kikiukaurujuani ya jua (Ultraviolet B-radiation) isifike kwenye uso wa dunia tunakoishi. Mwanzoni mwa miaka ya sabini, wanasayansi waligundua kwamba baadhi ya kemikali anazotengeneza binadamu na kuzitumia hujipenyeza angani na kumong'onyoa Tabaka la hewa ya Ozoni. Uchunguzi wa angahewa tangu miaka hiyo umethibitisha kuwa Tabaka la hewa ya Ozoni limekuwa likimong'onyoka kwa kasi ya asilimia tano (5) kila muongo.
Kemikali zilizotuhumiwa kuharibu Tabaka la hewa ya Ozoni ni pamoja na “Chlorofluorocarbons” (CFCs), na “Halons” ambazo zinatumika katika sekta za:-
Ø Viwanda – kutengeneza magodoro, viyoyozi na majokofu na usafishaji vyuma;
Ø Afya - kutengeneza madawa ya kupulizia (aerosols) kama vile X-Pel na manukato (Air freshner). Pia kutengeneza madawa ya kupulizia (inhalers) kwa ajili ya maradhi ya njia ya hewa kama vile pumu (asthma);
Ø Usalama - kutumika katika vifaa vya kuzima moto;
Ø Kilimo – kutumika katika ufukizaji wa udongo ili kuzuia wadudu waharibifu katika vitalu vya tumbaku, mashamba ya maua au hifadhi ya nafaka katika maghala.
2. Madhara yake
Matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya kikiukaurujuani (UV-B) kuifikia Dunia na kusababisha kuongezeka kwa:-
· magonjwa ya kansa ya ngozi;
· uharibifu wa macho kama vile "mtoto wa jicho" unaosababisha upofu;
· upungufu katika uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na madhara ya kujikunja kwa ngozi. Watoto wako katika hatari zaidi ya kupata madhara haya kutokana na uchanga wa miili yao; na
· athari katika michakato ya ukuaji wa viumbe hai na hivyo kusababisha mabadiliko katika mfumo na muundo wa viumbe hai katika ikolojia mbalimbali. Kwa mfano, katika ikolojia ya maji uzalishaji hupungua na vilevile mgawanyiko, ukuaji na kuzaliana kwa viumbe hai hubadilika.
3. Mikataba ya Vienna na Montreal

· Mkataba wa Vienna unahusu Kulinda Tabaka la hewa ya Ozoni na ulipitishwa mwaka 1985 na Mkataba wa Montreal unahusu Kemikali zinazosababisha kumong’onyoka kwa Tabaka hilo ambao ulipitishwa mwaka 1987. Mikataba hii inahusu dhamira ya Kimataifa ya kulinda Tabaka la hewa ya Ozoni angani.
· Kwa sasa kuna kemikali 96 zinazodhibitiwa na Mkataba wa Montreal.
4. Manufaa ya Mkataba kwa Tanzania:-
· Kulinda afya na mazingira kwa kuwa athari za mionzi hatari ya kikiukaurujuani (Ultra-Violet B radiation) haizuiwi na mipaka ya nchi hivyo watanzania kama walivyo wanadamu wengine duniani waweza kukumbwa na madhara ya mionzi;
· Kwa kutekeleza majukumu ya Mkataba, Tanzania imeweza kunufaika na tekinolojia mbadala za kisasa ambazo tayari zipo katika soko;
· Kuongeza uelewa wa wanasayansi nchini na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu umuhimu wa Tabaka la Ozoni kwa afya na mazingira;
· Kuongezeka kwa bidhaa salama katika soko la Tanzania;
· Kupata misaada kwa njia ya vifaa, mitambo na mafunzo kwa taasisi na sekta binafsi; na
· Kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika hifadhi ya mazingira hususan Tabaka la hewa ya Ozoni.
5. Mafanikio ya Mkataba
· Hadi kufikia mwaka huu utekelezaji wa Mkataba Duniani umewezesha kupunguza uzalishaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka la hewa ya Ozoni kwa asilimia tisini na tano (95 %).
· Vile vile upunguzaji huo umeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa gasi zinazochangia ongezeko la tabianchi.
· Tekinolojia na kemikali mbadala zimebuniwa na ziko katika soko.
6. Shughuli za mwaka huu
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Montreal Protocol - Global partnership for global benefits ” yaani Mkataba wa Montreal – Ushirikiano wa kimataifa kwa manufaa ya Dunia. Kauli mbiu inaonyesha umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kuhakikisha manufaa ya Dunia yanapatikana katika utekelezaji wa malengo yake. Kwa mfano, namna ambavyo Mkataba huu umesaidia kutekeleza Mkataba wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi. Baadhi ya kemikali haribifu hasa CFCs na HCFCs huchangia ongezeko la joto duniani hivyo kusababisha mabadiliko ya Tabianchi. Kwa hiyo kuondoshwa kwa kemikali hizo kumechangia kwa kiasi kikubwa upunguzaji wa gesi joto na madhara yake.
Katika kuadhimisha siku hii muhimu mwaka huu shughuli kuu ni kuelimisha wadau na jamii kwa ujumla:-
· kupitia vyombo vya habari kwa njia ya matangazo na makala;
· usambazaji wa vipeperushi; na
· Semina ya wadau katika Kanda ya Ziwa Victoria inayohusisha wawakilishi wa sekta binafsi kama vile Viwanda na karakana; TAMISEMI naTaasisi nyingine za serikali; na mashule na vyuo. Semina itakuza weledi wa wadau kuhusu hifadhi ya Tabaka la Ozoni na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake husika.
7. Changamoto katika kutekeleza Mkataba huu:-
· Utekelezaji wa Mkataba unahusisha wadau wengi hivyo kukuza weledi wa jamii ni changamoto mojawapo.
Ø Mikakati iliyopo ni kufikia wadau kwa makundi. Tumeanza na wafanya biashara na mafundi na taasisi husika za serikali. Tutaendelea na wadau wengine hasa jamii kwa ujumla;
Ø Njia zinazotumika kuwafikia wadau ni pamoja na usambazaji wa habari kwa njia ya redio, runinga (television), magazeti na makala mbalimbali. Pia semina za wadau, mafunzo na maonyesho ya bidhaa na vifaa vinavyotumia kemikali husika; na
· Changamoto nyingine ni kwamba Mkataba huu unahusu mabadiliko ya tekinolojia zinazotumia kemikali haribifu. Hivyo watanzania inabidi wawe wadadisi kujua bidhaa salama na vilevile wepesi kuendana na mabadiliko katika tekinolojia salama kimataifa ili kudhibiti athari za kiuchumi zinazoweza kusababishwa na mabadiliko hayo .
8. Wito
Natoa wito kwa wanamazingira popote pale walipo waendelee kuelimisha wananchi kuhusu athari za kuendeleza matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni na wahimize matumizi ya kemikali mbadala na bidhaa zake. Ni muhimu wafanyabiashara kuingiza nchini kemikali mbadala kwa wingi na bidhaa zake ili kudhibiti uingizaji holela wa bidhaa zisizohitajika.
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA

Toa Maoni Yako:
0 comments: