WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameondoka nchini leo (Jumanne, Septemba 30, 2008) kwenda Accra , Ghana kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) utakaoanza kesho Jumatano.
Waziri Mkuu Pinda anahudhuria mkutano huo akimwakilisha Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko nje ya nchi kikazi.
Huu ni mkutano wa sita wa Wakuu wa Nchi wanachama wa ACP, kati ya viongozi wa Afrika watakaohudhuria na kuhutubia ni pamoja na Rais wa Sudan, Omar El Bashir ambaye anamaliza muda wake kama Rais wa Mkutano wa 5 wa wakuu wa nchi za ACP.
Anayempokea El Bashir urais wa ACP na ambaye amepangwa kuhutubia katika mkutano huo wa 6 ni Rais wa Ghana , John Agyekum Kufuor.
Kati ya mambo muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huo wa Ghana ni yanayohusiana na usalama na maendeleo ya jamii.
Mengine yatakayojitokeza katika mkutano huo ni kupitia hatua iliyofikiwa katika malengo ya Milenia, kupanda kwa bei za vyakula katika nchi za ACP, masuala ya nishati, mabadiliko ya hali ya hewa na Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA).
Waziri Mkuu Pinda na ujumbe wake wanatarajiwa kurejea nchini Jumamosi, Oktoba 4, 2008.
Ends
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
DAR ES SALAAM
30.09.2008

Toa Maoni Yako:
0 comments: