Lile Tamasha kubwa la Kimataifa za nchi za Majahazi la Zanzibar (ZIFF) linaoendelea Zanzibar kwasasa, limeingia mkataba wa kusaidia kuanzishwa kwa tamasha kubwa la kitamaduni nchini Kongo baadaye mwaka huu. Taarifa hiyo imetolewa na Ofisa Mtendaji mkuu wa tamasha hilo, Dk Martin Mhando wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mtendaji huyo alisema tamasha lake limefurahishwa na nafasi hiyo kutokana na malengo yake ya kuwa na mtandao mkubwa wa sanaa utakaowezesha wasanii na wananchi kunufaika nao. Alisema mchango ambao unapelekwa kwenye tamasha hilo ni uzoefu na kitendea kazi muhimu katika uendeshaji wa tamasha, projekta.

Dk.Mhando alisema waandaazi wa tamasha la Kongo waliomba Africalia msaada wa mashine hiyo ambao waliwataka kuzungumza na ZIFF ambao tayari wanayo badala ya kwenda kuinunua kwa gharama ambayo ni kubwa.

Alisema ZIFF itapeleka mashine na fundi atakayesaidia katika shughuli nyingine za tamasha.

Kuanzishwa kwa tamasha la Kongo kutafanya idadi ya matamasha Afrika ya Mashariki na Kati yenye hadhi tofauti kufikia saba. Matamasha hayo yapo nchini Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, na la sasa la Kongo.Alisema pia mchango wao umelenga kufanikisha mawazo ya wasanii wa Afrika kuwa na mtandao mpana utakaoweza kutumiwa kwa ajili ya kukuza fikira, ubunifu na soko.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: