Licha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Abbas Kandoro na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kuwachimbia mkwara wasichana wanaojihusisha na biashara ya ukahaba jijini, hali imezidi kuwa mbaya kufuatia hivi karibuni wasichana waliodaiwa kuwa wanafunzi kunaswa wakijiuza katika maeneo ya Sinza.


Wanafunzi hao waliofahamika kwa majina ya Lucy na Husna wakazi wa Kinondoni, waliotajwa kuwa ni wanafunzi wa Chuo kimoja kikuu nchini (Jina kapuni) na mmoja ambaye ni denti wa sekondari moja ya wasichana jijini aliyetajwa kwa jina moja la Halima, walikutwa maeneo ya Sinza Afrikasana usiku wa Julai 14, mwaka huu wakiwa ‘mawindoni’.


Awali, mwandishi wetu aliyekuwa ameweka kambi maeneo hayo kufuatia taarifa ya kwamba, wanafunzi hao wamekuwa na tabia ya kufika eneo hilo kujiuza, aliwaona mabinti hao wakishuka kwenye teksi wakiwa wamevalia vinguo vya kibiashara hali iliyothibitisha yaliyokuwa yakisemwa.


Kama hiyo haitoshi, paparazi wetu aliwashuhudia mabinti hao wenye maumbo ya kimis wakijongea karibu na walipokuwa wamesimama machangudoa wenzao na kuanza kupiga stori.


Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuwafotoa picha wasichana hao lakini kabla ya kufanikisha zoezi hilo, baadhi yao walimshitukia na kuanza kumrushia mawe.


Aidha, baadaye mwandishi wetu katika pitapita yake alifanikiwa pia kukutana na warembo kadhaa katika eneo hilo hatari usiku wa manane (kama wanavyoonekana ukurasa wa mbele) ambao hawahusiki kabisa na biashara hiyo haramu ingawa haikuweza kubainika nini walichokuwa wakifanya katika eneo hilo maarufu kwa vitendo vichafu vikiwemo vya ukabaji.


Katika siku za hivi karibuni, gazeti hili limekuwa likifanya uchunguzi juu ya kushamiri kwa biashara hiyo haramu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Kandoro na kubaini kuwa, wanaofanya biashara hiyo wengi wao wanatoka katika familia duni.


Machangudoa hao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa ujasiri wa hali ya juu huku wakitumia mbinu kali za kuwakwepa ‘Vijana wa Mwema’ ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakiendesha msako kabambe wa kawakamata akinadadapoa.


Amani linaliomba jeshi la polisi kuongeza nguvu ya kupambana na wanaojihusisha na biashara hiyo hasa katika maeneo ya Sinza, Shekilango Road, Kinondoni, Oysterbay, Jolly Club, Buguruni,


Temeke na maeneo mengine yanayosifika kwa ukahaba kwani wamekuwa wakichochea kuongezeka kwa maambukizi ya Ugonjwa hatari wa Ukimwi-Mhariri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: