USAILI wa vijana katika zoezi la kusaka vipaji vya soka Vodacom Global Soccer Stars unafanyika kwa Mkoani Dar es Salaam linafanyika Ijumaa hadi Jumapili kwenye Uwanja wa Karume, Dar es salaam.

Meneja Masoko wa Vodacom, Emilian Rwejuna awali alitangaza kuwa usaili huu utafanyika uwanja wa zamani wa Taifa, lakini wameamua kupeleka Karume kwa sababu uwanja huo unatumika kwa Mashindano ya Kombe la Kagame.

Alisema zoezi hilo pia limefanyika katika mikoa ya Arusha , Mwanza, Zanzibar na Mbeya na vijana wengi wenye vipaji walijitokeza kwa wingi na kuwapa wakati mgumu makocha kuchagua
vipaji.

Alisema zoezi hilo linahusisha vijana wenye umri kuanzia miaka 16 na 22 na jumla ya vijana 40 wanatakiwa kutoka mikoa yote ambao ndio wataingia kambini katika Hoteli ya Collesium iliyopo
Oysterbay jijini Dar es salaam.

Zoezi hilo linafanywa na makocha wawili kutoka England ambao ni John Brookes na David Byrne na makocha 4 kutoka Tanzania wakiongozwa na Sunday Kayuni.

Alisema mwishoni atapatikana kijana mmoja nyota atakayejulikana ambaye ndiye atakuwa mwanasoka nyota wa Vodacom na moja kwa moja atapata nafasi ya kujiunga na chuo maalum ya mafunzo ya soka nchini Uhispania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: