Nikiwa na Mchomvu pande za Clouds Fm ndani ya XXL alikuwa akiwakilisha katika mkutano wa 50 Cent huku kipindi kikirushwa Live bila chenga kutoka pande hizo...

Nikiwa na wadau wetu upande wa usafiri Clouds Fm kilia ni Saidi na Alex katika mkutano wa 50 Cent huku vifaa vyangu vya kazi vikiwa mezani hapo nilikuwa nikijaribu kuwasiliana na ndugu na jamaa nikiwaelezea kuwa 50 Cent kashawasili ndani ya Dar es Salaam na muda mfuri ataongea nasi.

B12 (kushoto) na Mzee mzima Ruben wote hawa ni watangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha XXL ambacho ndicho chimbuko la 50 Cent kuja Dar es Salaam. Kipindi hicho kiliruka Live na kusababishwa na mtu mzima B12.

50 Cent akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari...
Mwanamuziki wa kimarekani 50 Cent akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari mara baada ya kutua jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni mwenzake Tony Yayo na mkurugenzi wa Clouds Fm pamoja na Prime Time promotion Bw. Joseph Kusaga ambaye alikuwa mwenyeji wao.

Kutoka kulia ni Kelvin Twisa meneja masoko wa kampuni ya simu za mkononi TIgo ambao ndiyo walikuwa wadhamini wa ujio huo, wengine ni Tony Yayo, 50 Cent pamoja na mkurugenzi wa Clouds Fm pamoja na Prime Time Promotion, Joseph Kusaga. Wakiwasilikiza waandishi wa habari wakati wakiuliza maswali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: