
Mwanamuziki nyota kutoka nchini Afrika Kusini Yvonney Chaka Chaka ambaye kwa sasa ameokoka na anaimba nyimbo za injili ametua leo mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusindikiza uzinduzi wa albamu mpya ya kundi la New Kitim tim inayaoitwa 'Vita hii yatoka Wapi' utakaofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho kuanzia saa 7mchana. Pichani ni Yvonne Chaka Chaka akifanya mahojiano na mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Jane mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wengine ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Anglican la mjini Dodoma, Dickson Chilongoni (kulia) aliyekuwa akifuatilia kwa makini mahojiano hayo.

Yvonne Chaka chaka akizungumza na baadhi ya wenyeji wake waliokwenda kumpokea uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo mchana, ambapo kulia ni mwanamuziki wa nyimbo za injili hapa mchini Bi. Upendo Kilahilo pamoja na Mama mchungaji Upendo Chilongoni wa kanisa la Anglican la mjini Dodoma ambalo linasimamia kwaya ya New Kitimu timu.
How do you play Barcelona in this year?
ReplyDelete