RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amani Abeid Karume ameondoka nchini leo kuelekea Uganda kwa ziara ya kikazi ambapo anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Karume ambae atakuwepo nchini Uganda kwa ziara ya siku mbili atashiriki katika ufunguzi wa msikiti mkubwa katika eneo la Kusini mwa jangwa la Sahara uliojengwa nchini Uganda pamoja na kuhudhuria katika maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) nchini humo.
Katika ziara hiyo Rais Karume amefuatana na viongozi mbali mbali wa dini na Serikali akiwemo Mhe. Burhani Saadat, Mhe. Ali Mzee Ali, Mhe. Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Ali Khatib Mranzi, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Harith bin Khelef, Sheikh Burhan Idd, Mhe. Abdulrahman Kinana, Sheikh Suleiman Gorogosi, Sheikh Fadhil Soraga pamoja na Sheikh Thabit Noman Jongo.
Habari kwa hisani ya Rajab Mkasaba kutoka Ikulu ya Zanzibar.

Toa Maoni Yako:
0 comments: