Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Bw. Godfley Kusaga wakizungumza na waandishi na jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mpambano mkali wa makundi mawili ya muziki wa kizazi kipya likiwemo kundi la Wanaume TMK Original na Wanaume TMK Halisi, na pia kuwatangaza rasmi wadhamini wa matamasha yote ya MKALI NANI, litakalofanyika April 11 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na baadae litaendelea katika mikoa nane. Kati ni Meneja masoko wa kampuni ya simu za mikononi ya TIGO Kelvin Twisa, ambao wametangaza kuwa wadhamini wakuu wa pambano hilo kwa mikoa yote wakifuatiwa na kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager.

Zikiwa zimebakia siku chache wale wapenzi wa muziki wa bongofleva kupata ladha waliyokuwa wameikosa kwa siku nyingi, meneja masoko wa kampuni ya simu za mikononi ya TIGO, Kelvin Twisa (katikati) wametangaza rasmi kuwa ndio wadhamini wakuu wa matamasha yote ya MKALI NANI yanayotarajiwa kuhusisha makundi mawili ya muziki wa kizazi kipya yaani TMK Wanaume Halisi na TMK Wanaume.
Inspector Harun akiwapa vionjo kidogo waandishi wa habari na kuelezea jinsi walivyojiandaa.
Kelvin alisema kuwa kampuni ya TIGO ndio mdhamini mkuu wa matamasha yote ya MKALI NANI kwa mwaka huu wa 2008, na aliongeza kuwa udhamini huo unalengo la kuhakikisha burudani ya makundi haya pamoja na muziki wa bongofleva unaendelea kuwa na burudani na upinzani mkubwa ili kuwavutia washabiki wengi hapa nchini na hata nje ya nchi.
Mheshimiwa Temba akieleza matarajio yake jinsi kundi lake lilivyojiandaa.
"Ni imani yetu kuwa udhamini wetu utatoa nafasi ya kutangaza umahiri wa kazi za makundi haya kwa jamii na kutoa changamoto kwa makundi mengine nchini kuendelea kujiandaa na kujipanga vizuri saidi, upinzani wa kujituma kufanya kazi nzuri uliopo kati ya kundi la Wanaume TMK Original na Wanaume TMK Halisi tunauhesabu kuwa ni sehemu ya burudani, na changamoto ya kufanya kazi zao zipendwe na mashabiki wengi, hivyo udhamini wetu utaifikia jamii kwa kuwaletea burudani ya kutosha kwa kipindi chote cha matamasha yatakayofanyika mkoani Dar, Dodoma, Morogoro, Arusha, Tanga, Mbeya, Mwanza pampoja na Zanzibar.
Pia Wasanii wanaochipukia watajifunza mambo mengi ikiwemo kujituma kisanii zaidi mara wawapo jukwaani kuwa kujifunza kutoka kwa wasanii hawa wa makundi mawili".
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: