Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew Juma Salum Yangwe (katikati), akizungumza na makada na wanahabari wakati akitangaza nia mjini Bagamoyo mkoani Pwani Pwani jana. Kushoto ni Meneja wa Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe na Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga.
 Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga(kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mzee Abdallah Ngumbe akizungumza katika mkutano huo na wakati akimpa ushauri mbalimbali mtangaza nia huyo.
 Profesa Sameheni Kejeli akizungumza katika mkutano huo.
 Mzee Hussein Lugome akizungumza katika mkutano huo.
 Mama mzazi wa mtangania huyo, Mary Yungwe akiwasalimia makada wa CCM katika mkutano huo.
 Mtangaza nia huyo akipongezwa na vijana baada ya mkutano huo.
 Pongezi zikiendelea.
 Mkutano ukiendelea.
---
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa amepata mpinzani baada ya kijana mdogo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Yungwe kutangaza nia ya ubunge katika jimbo hilo.

Akizungumza na makada wa CCM na waaandishi wa habari mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana, Yungwe alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ili kusukuma maendeleo ya jimbo hilo ambayo yamekwama kwa muda mrefu.

"Wanaccm wenzangu na wazee wangu nimeamua kugombea nafasi hii ili niwatumikie kwani Bagamoyo naelewa vizuri na nitaendelea kuwa wilayani hapa ili tushirikiane katika mambo mbalimbali ya nmaendeleo" alisema Yungwe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: