Watu wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya kutokea ajali ya barabarani baina ya basi la FM Safari na fuso ndani ya hifadhi ya wanyama ya Mikumi katika barabara kuu ya Iringa - Morogoro majira ya saa 5:30 asubuhi ya leo Machi 17, 2015 mkoani Morogoro.

Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni mwendo kasi uliochangiwa na dereva wa basi la FM Safari kushindwa kuwa makini wakati akiyapita magari mengine hali iliyolazimu kugongana uso kwa uso na fuso lililokuwa na dereva, abiria mmoja na utingo ambapo dereva na abiria walifariki dunia papo hapo huku utingo akijeruhiwa.

Dereva wa basi amevunjika mguu wa kushoto sambamba na mkono wa upande huo huku majeruhi wengeni 18 kati yao wakikimbizwa kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na St. Kizito.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: