TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUZO YA JAMII ITAKAYOTOLEWA TAREHE 13 APRIL 2015 KATIKA UKUMBI WA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE, JIJINI DAR ES SALAAM.

MGENI RASMI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete

WAGENI WAALIKWA:

Mara baada ya Hafla ya Tuzo ya Jamii ambapo Washindi wote watapewa Tuzo na Mgeni

Rasmi, Kutakuwa na Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii ambayo itahudhuriwa na
wageni wafuatao:




  • Wapewa Tuzo,
  • Familia za wapewa Tuzo,
  • Viongozi Waandamizi wa Serikali,
  • Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania,
  • Viongozi wa vyama vya siasa na kijamii na Wafanyabiashara,
  • Taasisi zisizo za kiserikali,
  • Watu Mashuhuri na
  • Wawakilishi kutoka makundi yenye
    mahitaji maalum ambapo kwa mwaka huu watawakilishwa na Watu wenye Ulemavu wa Ngozi - Albino.
MUHIMU:

Tanzania Awards International Ltd imepanga kufanya hafla ya utoaji wa Tuzo ya Jamii na kisha Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii siku ya tarehe 13 ya mwezi April ya kila mwaka kwa malengo ya kuadhimisha Kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa 
Baba wa Taifa,  Hayati Mwalimu Julius Kambarege Nyerere.

Kuhusu Tanzania Awards International Limited

Tanzania Awards International Limited ni kampuni iliyosajiliwa kisheria nchini Tanzania kwa Malengo ya Kufanya tafiti mbalimbali, Kutoa ushauri wa kisheria na kijamii, kuandaa na kuratibu matukio pamoja na Uandaaji na Utoaji wa Tuzo Ya Jamii.


Maana ya Tuzo ya Jamii.

Tuzo ya Jamii ni Tuzo inayotolewa kwa Taasisi na Watu binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zao katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.

Malengo ya Tuzo ya Jamii

Kutambua, Kuthamini, Kuunga Mkono na Kutoa Tuzo kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.
Kuikumbusha jamii kuona umuhimu, kujali na Kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi au Mtu Binafsi katika kuleta Ustawi na Maendeleo ya Jamii
VIPENGELE VYA TUZO YA JAMII 2015

Vipengele vya Tuzo ya Jamii, hubadilika kila mwaka kulingana na aina na matokeo ya

Utafiti unaofanywa na Tanzania Awards International Limited. Kwa mwaka huu
(2015), Tuzo ya Jamii itakuwa na Vipengele Vikuu vinne (4) vifuatavyo:

  1. Tuzo ya Jamii 2015
  2. Tuzo ya jamii –Tuzo ya Heshima
  3. Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu
  4. Tuzo ya Jamii kwa Mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania
UFAFANUZI WA KILA KIPENGELE CHA TUZO YA JAMII 2015

  1. Tuzo ya Jamii 2015
Tuzo hii itatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na mchango na jitihada zake

katika kusaidia na kutetea Jamii.

Mshindi wa Tuzo hii ya Jamii atapatikana kwa:

(a)   Mhusika mwenyewe kuwasilisha vielelezo au ushahidi wa mchango wake huo kwa Jamii


AU

(b)   Kwa jamii kupendekeza jina la mhusika kupitia mitandao ya kijamii

AU
(c)    Kwa Kamati ya Tuzo ya Jamii kufanya utafiti, kuchambua na kuteua jina moja miongoni mwa yale yaliyopatikana kupitia kipengele (a) na (b).

Mshindi wa Tuzo ya Jamii 2015 atatangazwa rasmi siku ya Hafla ya Tuzo ya Jamii

itakayofanyika tarehe 13 April 2015 katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre, Jijini Dar es Salaam.


2. Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima


Watakaopewa Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima ni:

(a)  Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na

(b) Hayati Nelson Mandela –Rais wa Kwanza Mzalendo wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini.

Tuzo hii ya Heshima kwa mwaka huu itatolewa kwa Waasisi hao wawili kutokana na Jitihada na Mchango wao wa kipekee na uliotukuka katika kutetea na Kulinda Maslahi ya Wanyonge.

3. Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu

Tuzo hii inatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika Kuelimisha, kulinda, kutetea na Kuimarisha Utawala Bora nchini Tanzania.

Vigezo vinavyotumika kwa mwaka huu katika kumpata mshindi wa Tuzo ya Jamii ya Haki za Bianadamu, ni hivi vifuatavyo:

Weredi wa Taasisi au Mtu Binafsi katika kufanya uchunguzi, Utafiti na kutoa taarifa zake kwa uhuru, pasipo upendeleo wowote kwa Serikali, Chama, Kikundi au mtu Binafsi
        
Mchango wa Mtu Binafsi au Taasisi katika Kuelimisha Jamii,  kulinda, kutetea na kuhamasisha juu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania.

Mchango wa Mtu Binafsi au Taasisi katika kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha juu Amani, utulivu, Usalama wa Raia na Mali zao na Utii wa Sheria kwa ujumla

  1. Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania
Mshindi wa Tuzo hii atatangazwa siku ya hafla ya Tuzo ya Jamii baada ya mwanasiasa husika kupigiwa kura nyingi kupitia mtandao wa Push mobile ambapo mpigaji wa kura anatakiwa aende sehemu ya kuandika ujumbe mfupi wa maneno  katika simu yake ya Mkononi na kuandika namba ya Mwanasiasa husika, halafu  anatuma namba hiyo kwenda 15522.


Vigezo vitakavyotumiwa na wapiga kura kupitia namba 15522 ni hivi vifuatavyo:


  • Uadilifu, Uaminifu, Heshima na Utii kwa Jamii na sheria za nchi kwa Amani ya nchi yetu
  • Jitihada binafsi katika kulinda na kutetea Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar, Umoja wa Kitaifa na Kijamii.
  • Uzoefu wa Uongozi wa Umma, Taasisi za Kimataifa na Mchango wake kwa Jamii.

  • Matarajio, Mipango na nia ya Dhati ya Kuleta Maendeleo na Mafanikio kwa Watanzania.
Orodha ya Wanasiasa wanaowania Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Kijana na Mtu Mzima Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania imepatikana baada ya wanajamii kupendekeza mara nyingi jina la Mwanasiasa husika kupitia Mtandao wa Push Mobile na mitandao mingine ya kijamii. Kamati ya Tuzo ya Jamii, 
baada ya kupitia majina yote yaliyopendekezwa kupitia mbalimbali ikiwemo Push 
Mobile, imepata orodha ifuatayo:
WATU WAZIMA



JINA LA MWANASIASA


NAMBA YA KUMPIGIA KURA


MHE. MIZENGO PETER PINDA


MM01


MHE. PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO


MM02


MHE. DR. WILBROD PETER SLAA


MM03


MHE. ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO


MM04


MHE. SAMIA HASSAN SULUHU


MM05


MHE. JAMES FRANCIS MBATIA


MM06


MHE. DR. JOHN POMBE MAGUFULI


MM07


MHE. DR. HARRISON GEORGE MWAKYEMBE


MM08


MHE. PROF. IBRAHIM HARUNA LIPUMBA


MM09


MHE. STEPHEN MASATU WASIRA


MM10


MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA


MM11


MHE. BENARD KAMILIUS MEMBE


MM12


MHE. EDWARD NGOYAYI LOWASSA


MM13

VIJANA



JINA LA MWANASIASA


NAMBA YA KUMPIGIA KURA


MHE. JANUARY YUSUPH MAKAMBA


MK01


MHE. ZITTO ZUBERI KABWE


MK02


MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA


MK03


MHE. HALIMA JAMES MDEE


MK04


MHE. SAADA SALUM MKUYA


MK05


MHE. LAZARO SAMUEL NYALANDU


MK06


MHE. ESTHER AMOS BULAYA


MK07


MHE. UMMY ALLY MWALIMU


MK08


MHE. NAPE MOSES NNAUYE


MK09


MHE .MBONI MHITA


MK10


MHE. DAVID ZACHARIA KAFULILA


MK11


MHE. VICKY PASCHAL KAMATA


MK12


MHE. JOHN JOHN MNYIKA


Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: