Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe wa pili   kushoto na viongozi wa Halmashauri  wakikabidhiana daraja la mto Kitewaka kwa  ajili ya  kujengwa kisasa baada ya  serikali  kukabidhi fedha za ujenzi huo Tsh miloni 240
 Mbunge  Filikunjombe akilitazama daraja la mbao la mto Kitewaka ambalo litajengwa  kisasa.
 Wannchi  wa  kijiji  cha Maholong'wa  wakimpongeza  mbunge  Filikunjombe kwa kutimiza ahadi yake.
 Waumini  wa  kanisa la Anglikana Maholong'wa Ludewa  wakimkabidhi zawadi mbali mbali mbunge Filikunjombe baada ya  kuwasaidia bati na  saruji  ya kutosha  kujenga kanisa  jipya.
 Viongozi wa kanisa la Anglikana na wa CCM Ludewa  wakiongozana na mbunge Filikunjombe  mwenye kofia.
 Mbunge  Filikunjombe akisaidi kupalilia mahindi katika shamba la mchungaji wa kanisa la Anglicana Maholong'wa baada ya  kufika  kusaidia ujenzi  wa kanisa  hilo.
 Mkutano wa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe na  wanakijiji  wa Maholong;wa.
 Mzee  wa  kanisa la E.A.G.T Maboga  Ezekia Mhagama (kulia)akimwombea dua  mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya  kutoa misaada  mbali mbali ya ujenzi na  kujitolea kinanda  kwa  kanisa  hilo vyote  vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11  wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maholong'wa.
---
Na matukiodaima Blog.

MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ametimiza ahadi yake ya ujenzi wa daraja la mto  Kitewaka katika kijiji cha Maholong'wa kata hiyo ya Ludende baada  ya serikali kumpatia  kiasi cha Tsh milioni 2480 zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya ujezi wa daraja hilo .

Mbali ya  kutimiza ahadi hiyo ya  daraja  pia amechangia vifaa vya ujenzi vyeye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Maholong'wa na ujenzi wa kanisa la Anglikana kijiji cha Maholong'wa kata ya Ludende wilayani Ludewa mkoani Njombe .

Akizungumza na wananchi hao leo mbunge Filikunjombe alisema kuwa kuwepo bungeni ni heshima ya wana Ludewa na kuwa hata vurugu kubwa ambazo amekuwa akizifanya bungeni si kwa maana nyingine zaidi ya kupigania maendeleo ya wananchi wake.

Hata   hivyo  aliipongeza  serikali  kuwa  kusaidia  kutoa  fedha   hizo  kwa  wakati kwa ajili ya  kuanza ujenzi hao na  kuwa  iwapo  asingefuatilia kwa karibu   serikalini ama angekuwa wa kulala bungeni yawezekana  fedha kwa  ajili ya ujenzi wa daraja   hilo zisingetolewa sasa.

“Wapo wabunge wengine ambao kazi yao ni kusinzia tu na wala haulizi swali …..ila huo pia ndio uwakilishi wake ulipoishia …..mimi silali kule bungeni mimi ninawatetea na kuwapiganieni kwa kulia nalia na kwenye kugombana nagombana pia pale kwenye kunyenyekea nanyenyekea….. napenda kuwaelezeni kuwa kazi ambayo mlinipa kuwawakilisha bungeni naitumia vema hadi sasa sijakwama kuwatumikia ….nilisema mwanzoni mimi navurugu bungeni ila ni vurugu za kimaendeleo”


Filikunjombe alisema kuwa waakati akiomba kuwa mbunge wa Ludewa alitaka 

wawakilisha bungeni na kushirikiana nao katika shughuli za kimaendeleo hivyo angekuwa mbunge wa ajabu kama angekuwa mbali na shughuli za kimaendeleo katika jimbo lake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: