- Ni kawaida anapohitimu masomo hukaa tu nyumbani kusubiri ajira pasipo kujali changamoto za ajira.
- Kama ana ajira hafikirii tena njia mbadala za kujiongezea kipato. Suala la MADENI/MIKOPO kwake ndiyo njia mbadala ya kujiongezea kipato.
- Hana kazi lakini ni kawaida kukaa ndani akiangalia na kubadilisha movie hata kutwa nzima lakini hafikirii kujiajiri
- Ni kawaida kutumia simu kali "SMART PHONE" ht ya laki 5 lakin ukimgusia suala la kufanya biashara/Ujasiriamali atakwambia hana mtaji
- Ni kawaida kuhudhuria matamasha na makongamano ya BURUDANI tu tena kwa kuingia gharama lakin semina ya Ujasiriamali haendi japokuwa ni BURE.
- Anapenda kila kitu kiwe rahisi, hata akianza biashara anataka siku ya kwanza tu afanikiwe.
- Ni bingwa wa kulaumu Serikali kuhusu ukosefu wa ajira, lakini akipewa nafasi ni kawaida kuichezea.
- Hana kazi, hafanyi biashara lakini anapenda maisha mazuri tu. Sijui ni maisha gani mazuri unayoweza kuyapata pasipo kujishughulisha!
NAKUMBUKA USEMI WA RAIS WETU USEMAO "UKIPENDA KULA VYA WATU NI LAZIMA NA WEWE UKUBALI KULIWA" maana yake anataka watu tukubali kujishughulisha.
- Kila siku ametawaliwa na neno " NITAFANYA" badala ya neno "NAFANYA"
HAO NDIO SISI WATANZANIA.

No comments:
Post a Comment