Pages

Wednesday, 28 May 2014

WANAHABARI WAJITOKEZA KUMUAGA MWENZAO, MAREHEMU MAXMILIAN NGUBE JIJINI DAR

Jeneza lililohifadhi mwili wa Marehemu Maxmilian John Ngube likiwa kwenye viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam mchana wa leo Mei 28, 2014 tayari kwa shughuli ya kuagwa na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni. Max Ngobe alifariki Dunia mwishoni mwa wiki iliyopita kutoka na maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Risala fupi ikisomwa wakati wa Shughuli hiyo na Kuangwa kwa Marehemu Max Ngobe mmoja wa wanahabari wakongwe Tanzania.

Wanahabari wakirekodi tukio la kuaga Mwili wa Marehemu Max.

Sehemu ya waombolezaji wakiwa kwenye foleni ya kwenda kuaga mwili wa Marehemu Max.

Wengine leo ndiyo ilikuwa siku ya kukutana...
Sehemu ya Wadau wa Habari waliohudhulia shughuli hiyo.


Ankal akiwa na baadhi ya wanamuziki waliofika kwenye mazishi hayo.

Wasanii nao hawakuwa nyuma kuungana na wanahabari katika kumuaga mpendwa marehemu Max.
 Waombolezaji wakiwa na nyuso za simanzi.

Mwili wa Marehemu Max ukielekea Makaburi ya Kinondoni kwa Mazishi.
Waandishi wa Habari wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mpigapicha wa Mlimani TV, Marehemu Maxmillian John Ngube, wakati wa hafla ya kumuuaga iliyofanyika katika viwanja vya Klabu ya Leaders jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akitoa heshima za mwisho.
Wasanii wa Bongo Movie na Wanamuziki kutoka Bendi Mbalimbali walihudhuria.
Mtoto wa Marehemu Max, Jacob akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa baba yake.
Mtoto wa Marehemu Max, Rose akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa baba yake.
Mjane wa Marehemu, Bi. Suzan Jacob Ayimba akiuaga mwili wa mpendwa mme wake.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Max (pichani) likiondolewa katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kupelekwa katika makaburi ya Kinondoni kwa Mazishi.

No comments:

Post a Comment