Na Hellen Kwavava, Dar es Salaam.

Waziri wa kilimo, chakula na ushirika CHRISTOPHER KAJOLO amesema kuwa hali ya uzalishaji wa chakula katika maeneo mbalimbali nchini imepanda hadi kufikia asilimia 118 kutoka mwaka 2013/2014 hivyo kulifanya taifa kuwa na chakula cha kutosha.

Akiongea na waandishi wa habari Waziri KAJOLO Ameeleza kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa kilimo wa mwaka 2013/2014 ni tani 14.41 za chakula zikiwemo tani 7.6 za nafaka na tani 6.86 za mazao yasiyo ya nafaka.

KAJOLO amesema kuwa serikali imedhamiria kuongeza uzalishaji wa mazao ya nafaka katika mikoa mbalimbali nchini.

Ameeleza kuwa kwa sasa imejipanga kuanzisha kilimo cha mpunga na sukari chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) ili kuliwezesha taifa kuinuka na kukua kiuchumi.

Hata hivyo serikali imejipanga kupeleka miundo mbinu na pembejeo za kutosha vijijini ili ziweze kuwasaidia wananchi katika kilimo ili waweze kutoka katika hali ngumu ya maisha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: