Washiriki wa mkutano wa 7 wa Mapitio ya Utendaji wa sekta ya
Uchukuzi, wakijitambulisha kabla ya mkutano huo wa siku mbili kuanza
katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jubilee. Mkutano huo wa 7
unawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Uchukuzi kujadili changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka
akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano 7 wa mapitio ya utendaji wa
Sekta ya Uchukuzi(JTSR 2013), unaofanyika katika ukumbi wa mikutano
Jengo la Golden Jubilee tarehe 28-29 Oktoba 2013. Mkutano huo wa 7
unawakutanisha wadau mbambali wa sekta ya uchukuzi kujadili changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya uchukuzi na kuzitafutia ufumbuzi ili
kuboresha Uchukuzi nchini Tanzania.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa sekta ya Uchukuzi
leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye Jengo la Golden
Jubilee(PSPF BUILIDNG). Mkutano huo wa siku mbili unakutanisha wadau wa
taasisi mbalimbali za sekta ya uchukuzi kujadili njia mbalimbali za
kuboresha sekta ya Uchukuzi.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kushoto
waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi, wahisani wa Miradi
ya Maendeleo na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano wa 7 wa mapitio
ya utendaji wa sekta ya Uchukuzi, Unaofanyika tarehe 28-29 Oktoba
katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Golden Jubilee. Wa kwanza kushoto
waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs. Monica
Mwamunyange, kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.
(Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)


Toa Maoni Yako:
0 comments: