Mambo
makubwa yamefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba usiku huu jijini
Mwanza ambapo Mwanamuziki Gwiji la miondoko ya bolingo, Barani Afrika kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo Kofii Olomide akiwa na kundi lake amepagawisha mashabiki wa muziki
wake katika tamasha la Tusker Carnival .
Mwanamuziki Kofii Olomide amefanya mambo
makubwa kama alivyoshusha burudani jana kwenye viwanja vya Leaders
jijini Dar es salaam, Watu mbalimbali wamiminika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba ili kumuona mwanamuziki huyo (pichani juu) akiwa na first lady wa bendi hiyo mwanamama Cindy aliyetambulishwa kwa mashabiki wa jijini
Mwanza.
Kofii Olomide akiimba huku akiwa amezungukwa na wanenguaji wake
Mwanamuziki Cindy katikati Mwimbaji mahili wa mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani kalba ya Kofii kupanda jukwaani.
Kazi iko hapa kama wanavyoonekana wanenguaji hao wakicheza kwa staili mpya.
Hii ilichezwa kwa kwenda mbele na kurudi nyuma huku wakiwa wameshikana.
Palikuwa hapatoshi kwa shoo kabambe.
Ili mradi burudani iliyopangika kutoka kwa wanenguaji hao
Ilichezwa kwa hisia pia
Kutoka
kulia ni Ephraim Mafuru, Anitha Msangi Maurice Njowoka na Patrick
Kisaka kutoka kampuni ya bia ya Serengeti wakishoo love kwa picha.
Wadau kutoka Miss Tanzania wakiwa katika onesho hilo.
Rachel wa THT akicheza na mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide.
Kofii Olomide akimpongeza msanii Rachel wa THT baada ya kuonyesha uwezo wake katika kuimba kwenye onesho hilo.
Rapa
wa mwanamuziki Kofoo Olomide anayejulikana kwa jina la Computar
akighani jukwaani huku wanenguaji wa kiume wakiingia jukwaani.
Pepe Kale wa Mwanza naye akaifanya mambo makubwa na kukubalika na umati wa mashabiki waliohudhuria katika onesho hilo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: