Waziri wa maliasili na Utali Mh. Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika uzinduzi wa Mkakati wa mpya wa Utangazaji wa Kimataifa wa Utalii wa Tanzania (International Marketing Strategy For Tanzania)mpango uliozinduliwa jioni hii na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kujumuisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya utalii ambapo Waziri Kagasheki ameuzindua rasmi.
(PICHA NAWWW.FULLSHANGWEBLOG,COM)
Waziri wa maliasili na Utali Mh. Balozi Khamis Kagasheki akikata utepe katika kitabu kinachoelezea mkakati wa kutangaza utalii wa utalii wa Tanzania kimataifa kutoka kulia ni Bw. Gaudence Temu Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Ahmad Khatib Kamishna wa Utalii na kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dkt. Aloyce Nzuki.
Bw. Gaudence Temu Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT) akielezea mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa kwa wadau wa masuala ya utalii waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Mbunge wa Mafia na Mjumbe wa Bodi ya (TTB) Mh. Abdulkarim Shah
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Utalii Tanzania TCT Bw. Richard Rugimbana kulia akijadiliana jambo na Dan Kisirye kutoka International Finance Corporation, katikati ni Godfrey Simbeye Mkurugenzi Asasi ya Sekta Binafsi Tanzania Private Sector Foundation.
Kutoka kulia ni wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTBKaraze, Beatrice na Fatma wakiwa katika picha ya pamoja.
Kundi la Wanne Star likitumbuiza katika uzinduzi huo
Baadhi ya maofisa wa bodi ya utalii Tanzania wakiwa katika hafla hiyo wakibadilishana mawazo hapa na pale kulia ni Bw. Mussa Kopwe Mkuu wa Utawala, Bw. Deo Mkuu wa Utafiti kushoto na Bw. Kaduma Mwanasheria wa (TTB) katikati.


Toa Maoni Yako:
0 comments: