Pichani ni Bw. Athuman Hamisi ambaye ni Mpiga Picha wa magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper (Sunday News, SpotiLeo, Daily News na Habari Leo) akiongea na waandishi wa habari juu mustakabali wa maisha yake tokea amepata ajali ya gari. Athuman ambaye alipata ajali ya gari Septemba 12.2008 katika eneo la Kibiti mkoani Pwani na kupelekea kuvunjika shingo na kudamage spinal cord hali inaliyopelekea kupooza mwili mzima hivi sasa yuko katika hali ngumu ya kimaisha ambapo anahitaji wasamaria wema kumsaidia ili aweze kukabiliana na ukali wa maisha.

Alisema kuwa, "Nimekuja leo kuutangazia Umma hali ilivyo. Ukweli kwa sasa account yangu ya CRDB ilikuwa maalum kwa ajili ya kusomeshea watoto, imekauka ya Postal Benki ambayo ya mshahara haina kitu. Pesa ya mshahara inayoingia benki ni 450,000/-


Namlipa nurse na msaidizi wake na mfanyakazi kiasi cha tshs. 370,000/-. Maisha ya ulemavu ni ghali sikutarajia. Nina wanangu watatu, wa kwanza anamaliza darasa la Saba mwaka huu, wa pili yuko la nne na wa mwisho huko darasa la pili.

Hawa wanaosoma shule ya msingi niza kulipia 200,000/- kula term jumla 400,000/- hizo shule zina term nne kila mwaka. Gharama chakula, vifaa vya wanafunzi, gharama zao ndogo ndogo na za kifamilia pamoja na chakula kwa mwezi, inakwenda kati ya 750,000/- mpaka 900,000/- kwa mwezi.

Nimekuwa omba omba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei simu wala kujibu sms. Siyo siri, ndugu wote wamekimbia waliobaki ni marafiki wa kweli wamenitangazia katika familia zao. Hali yangu ni mbaya sana kiuchumi.

Sina uwezo wa kulipia nyumba kwa gharama zozote zile. Mimi Athuman Hamisi naomba watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa nyumba na ushauri wa madaktari walionishauri nisiishi mbali na mazingira ya hospitali kulingana na hali yangu.

Makampuni, Mshirika, Wizara yoyote, Shirika la Nyumba la Taifa NHC, Watu binafsi, Serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu nawaomba wanisaidie kwa nia yoyote. Kwa walio tayari naomba misaada ipitie katika account ya CRDB no; 01J2027048800 na Account ya Postal Benki no; 010-00090488.

Kwa wanaotumia mitandao ya simu wanaweza kutumia M-Pesa 0757825737, Tigo Pesa 0655531188 na Airtel Money 0784531188. Au unaweza kumtumia rafiki yake Bw. Chris Mahundi M-Pesa 0767298888, Ephraim Mafuru Airtel Money 0686710977.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. JAMANI HUYO JAMAA ALIPATA AJALI AKIWA KAZINI NA AMEFANYIA KAZI KWENYE JAMII ZETU,SEREKALI YETU SIJUI NI KWANINI INAPENDA KUSAIDIA MTU AKISHAKUFA,WANAMPA MAMA KANUMBA MILIONI KUMI,ZA NINI ZOTE HIZO??NI KWANINI WASIMSAIDIE HUYU MPIGA PICHA WA SEREKALI...MIE NASHANGAA SANA HII SEREKALI YETU,HIZI LAWAMA ZITUMWE SEREKALINI,SIO KUSAIDIA WATU WALIOKUFA....KANUMBA ALISHA KUFA,HIZO HELA MNAMPA MAMA YAKE ZA NINI???MDAU SWEDEN

    ReplyDelete