----
Vijana nchini wameshauliwa kuheshimu muziki wa hip hipo na kuuchukulia kama ni kazi na kujikita kujifunza maadili ya muziki huo ili waweze kusonga mbele na kupata mafanikio.
Hayo ameyasema mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 jijini Dar es Salaam Ruben Ndege katika mchakato wa kumtafuta mkali wa freestyle linaloendelea jijini Mbeya katika ukumbi wa Vibe, alisema kuwa kama kweli vijana wanahitaji kuwa wanahip hop wanatakiwa kujifunza maadili ya muziki huo.
"Msione wanamuziki wengi wa hip hop wamefanikiwa waliuheshimu muziki huo na kufuata maadili yake hivyo vijana acheni kuudharau muziki wa hip hop fanyeni kazi na mtaona mafanikio yake,"
Zoezi la kumtafuta mkali wa freestyle katika Serengeti Fiesta Freestyle leo limeisha kwa kupata vijana wapatao 15 ambao wameingia hatua ya pili hapo kesho katika ukumbi wa Vibe jijini Mbeya.


Toa Maoni Yako:
0 comments: