WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Idara ya Habari - MAELEZO, S.L.P. 9142 - DSM, Simu 2122771/3,
Fax: 2113814, Mob 0754234441
E-mail: maelezopress@yahoo.com
DATE: 15/09/2008
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara, Pius Msekwa amesema kwamba dekmokrasia nchini itadumishwa ikiwa kila mtu atakuwa na uelewa juu ya suala hilo .
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku Kimataifa ya Demokrasia , ambapo kauli mbiu ni “tuimarishe an kulinda Demokrasia Tanzania ”, iliyofanyika jana katika viwanja vya mnazi mmoja, Dares Salaam Msekwa alisema dekmokrasia inaweza kukuzwa kwa njia mbili ambazo zikitumika vizuri zitaiendeleza na kuidumisha.
“Mimi ninashauri kwamba tunaweza kudumisha demokrasia kwa njia mbili, ya kwanza ni kukuza uelewa wa demokrasia yenyewe. Pili kwa kutumia miundombinu vizuri ya demokrasia ya nchi. Tukielewa hivyo tutakuwa tuko sahihi katika kukuza demokrasia,” alisema Msekwa.
Msekwa akifafanua kuhusu miundombinu hiyo aliitaja kuwa ni Katiba ya Nchi na Sheria ya Serikali za Mitaa.
“Ni muhimu kutumia vizuri Katiba ya Nchi yoyote ndio inaweka misingi ya utawala wa nchi, serikali, Bunge, mahakama jeshi na usalama wa taifa.Tumekubali kuwa Katiba sio Msahafu inaweza” ikabadilishwa kulingana na mahitaji ya wakati huo,”alisema Msekwa.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema demokrasia ni nguzo muhimu ya kuleta haki za binadamu na nyenzo ya maendeleoa,hivyo misingi yake lazima iwekwe vizuri. Hata hivyo alilamikia kuhsu kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Oscar Fernandez –Taranco, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuimarisha demokrasia nchini.
Alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni uimarishaji wa demokrasia katika utawala bora na uwajibikaji , kuimarisha mijadala ya wazi ya kisiasa na kusaidia asasi za kiraia na vyombo vya habari vinavyozungumzia suala hilo.
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia(TCD), John Cheyo, alisema mfumo wetu sheria bado una mapungufu ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kukwanza kuimarika kwa demorasia, mfumo wa uchaguzi wa wengi wape unahallalisha sauti za wachache kubaki nje na wanawake bado wako nyuma katika eneo hilo.
Alisema hizo ni changamoto ambazo zinahitaji kurekebishwa.


Toa Maoni Yako:
0 comments: