Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, kabla ya safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera wakati wakielekea kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero leo.Watatu Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi (kushoto) na Mkewe Mama Sitti Mwinyi (katikati) wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa (kulia) kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo,Muhashamu Salitaris Melchior Libena iliyofanyika leo Ifakara,Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.
 Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akiongoza ibada yake ya kwanza akiwa ni Askofu wa Jimbo Jipya la Ifakara mara baada ya kusimikwa leo.
 Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa Viongozi wa Serikali waliohudhulia Sherehe hizo za kusimikwa kwake leo.
Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa wageni mbali mbali waliohudhulia Sherehe hiyo, wakiwemo waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa salamu kwa wakristo waliofika kwenye Sherehe hizo leo,ambapo ameliomba Kanisa Katoliki kuisaidia serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi akihutubia kwenye Sherehe hizo.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo mara baada ya kumalizika kwa Sherehe ya Kuzindua Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo iliyofanyika leo Ifakara,Mkoani Morogoro.
Mh. Lowassa akibadirishana mawazo na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono wakazi wa Ifakara.

Mh. Lowassa akizungumza na Mmoja wa wananchi wa Mji wa Ifakara.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono.
Waimbaji wa bendi ya Machozi wakiongozwa na Sam Machozi wakiimba ndani ya Nyumbani Lounge usiku wa kuamkia jana.
Mwanadada Lina wa Machozi Bendi akiwasha moto pamoja na Sam.
Mwanamuziki wa Machozi Bendi Joniko Flawa... akiwasha moto
Mwanadada Caroline akijiachia kwa raha zake.
....Mwanadada huyu anaimba sana, Mwenyezi Mungu amjalie azidi kukua zaidi na zaidi.
                                                                Lady Jay Dee  binti Machozi akiwasha moto
                                         Mwanadada Lady Jay Dee akipewa sapoti na Joniko maua mauaaaaaaa
Wapenzi wa machozi bendi walivyokuwa wakijiachia.
Tumba limekoleaaaaa
Ah! utamu wote unanogeshwa na hawa watu...
...Ehe! mambo yote yapo hapa, huyu jamaa ni hatari sana kwenye kukopiiiiiii dah! balaa sana
...hakuna haja ya kumsahau huyu jamaa ambaye yeye anahakikisha kila kitu kinatoa sauti inayotakiwa. Hongera sana kaka!
Moto ni ule ule kupenda ni kule kule..... malizia mwenyeweeeeeee
....muziki umekolea ila mtu na wake
....Mkali wa kuimba muziki wa regge
...Uhondo wote wa kuserebuka huwa unatoka hapa... huyu bwana ni mkali sana
Kijana machachali ndani ya Machozi bendi, Sam akionyesha vitu vyake
Akina dada wakijiachia
Komandoo Hamza Kalala alikiimba na mwanadada Lady Jay dee wimbo wa Nimekusamehe lakini sitokusahau, Visa ulivyonitendea Kalala eeeeeeeeeeeeh eeeeeeeeeh... Kwa sasa wimbo huyo amepewa mwadada huyo na anatarajia kuurudia kuuimba.
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia viatu na kusikiliza maelezo kuhsu utengenezaji wa bidhaa hiyo kutoka kwa Deogratias John (kushoto)  wa Chuo cha Waleavu cha Usariva Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa Deogratias Kessy wa banda la VETA Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA mkoa wa Tanga, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Tangamano, Kwa ajili ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na mwasisi wa Chuo cha Gemmologiacal and jewelry Vocation cha Arusha, Peter Salla, kuhusu matumizi yam awe ya madini, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua mashine ya king’ola kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa, amewataka wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.


Mh Lowassa aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi na viongozi wa shule ya sekondari ya wasichana ya mtakatifu Anns iliyoko Morogoro.




Aidha Mh Lowassa alitoa zawadi ya mpira kwa kila darasa katika shule hiyo, ikiwa ni katika kuhamasisha michezo mashuleni.

Naye Mkuu wa shule hiyo Sister Dennis pamoja na wanafunzi na watawa wengine shuleni hapo walimtakia Mh Lowassa afya njema ili aweze kuendelea kuwatumikia watanzania.
Katika picha Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro,Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro,Sista Martha (kushoto) wakati akiwasili shuleni hapo.Kulia ni Mke wa Mh. Lowassa,Mama Regina Lowassa na wa pili kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo,Sista Dennis.
Wanafunzi wa Shule ya Sekindari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Mh. Waziri Mkuu Mstaafu.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro