Mkazi wa Kijitonyama Cloud Opson (29) akizungumza na mshereheshaji wa Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash mara baada ya kutembelea promosheni ya “Fanyakweli Kiwanjani” kwa baa zilizo kwenye mkondo mmoja ambayo ilifanyika Banana-Ukonga jijini Dar es salaam wikiendi iliyopita. Baa hizo ni pamoja na:-Airtel, Serengeti, Blue Sky na Smart. (Kulia) ni Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ukonga na Chanika Tesha Stanslaus na kushoto ni balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi.
 Mkazi wa Majohe (Kwa ndevu) na mpenzi wa bia ya Tusker Catherine John akiizungumzia bia hiyo na kutaja sababu za kwanini anaifurahia wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ambayo wiki hii ilifanyika katika baa zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa ujumla zilitangazwa kama baa za wiki kwenye promosheni hiyo iliyofanyika Banana Ukonga jijini Dar es salaam wikiendi iliyopita. Baa hizo ni pamoja na:-Airtel, Serengeti, Blue Sky na Smart. (Kulia) ni mkazi wa Banana Eva Fred, (Kushoto) ni Balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi, Mshereheshaji wa Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash na balozi wa bia hiyo Mariam Ally.
Mkazi wa Majohe (Kwa ndevu) Catherine John akiifurahia zawadi yake ya fulana kutoka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti Tesha Stanslaus (kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ambayo wiki hii ilifanyika katika baa zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa ujumla zilitangazwa kama baa za wiki kwenye promosheni hiyo iliyofanyika Banana Ukonga jijini Dar es salaam wikiendi iliyopita. Baa hizo ni pamoja na:-Airtel, Serengeti, Blue Sky na Smart. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash.
Mtumbuizaji toka kikundi cha burudani na uigizaji “Cash dollar” cha Machimbo-Jet Rumo jijini Dar es salaam Salome Elly akionyesha ufundi wake stejini wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ambayo wiki hii ilifanyika katika baa zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa ujumla zilitangazwa kama baa za wiki kwenye promosheni hiyo iliyofanyika Banana Ukonga jijini Dar es salaam wikiendi iliyopita. Baa hizo ni pamoja na:-Airtel, Serengeti, Blue Sky na Smart.
---
Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani imeendelea kuzifikia baa mbalimbali jijini Dar na mikoani ambapo kwa mara nyingine tena promosheni hiyo imekuja kitofauti zaidi kwa wiki hii baada ya kuzifikia baa zaidi ya nne za jijini Dar es salaam.

Baadhi ya baa zilizoshiriki kwenye promosheni hiyo kwa wiki hii ni pamoja na:-Airtel, Serengeti, Blue Sky na Smart zote za Banana-Ukonga jijini Dar es salaam.

Promosheni hiyo ilianza kutimua vumbi kwenye viwanja hivyo kuanzia mida ya saa kumi jioni ambapo kama ilivyo ada burudani ya muziki ilisimamiwa vilivyo na MaDjs na washereheshaji kutoka redio E-fm ambao ni wadau wa Kampeni hii tokea kuanzishwa kwake.

Baadhi ya wateja waliojipatia zawadi mbalimbali kama fulana na bia za bure wakati wa promosheni hiyo mmoja wao ni Paul Ndenjemba (49) ambaye alifunguka na kusema kuwa ameanza kuitumia bia ya Tusker tangu mwaka 1995 na hajawahi kufikiria kuiacha bia hiyo kwa kuwa haimchoshi na akiamka asubuhi anawahi kwenye shughuli zake kama kawaida.

Aliupongeza uongozi mzima wa bia ya Tusker na kusema promosheni kama hizi zinawaleta wateja karibu na kuwafanya wajione wenye fahari kutokana na uwepo wa bia inayowajali wateja wake.

Kwa upande wake Meneja masoko wa bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella alisema “Sherehe za baa zilizo kwenye mkondo mmoja huiwezesha promosheni hii ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani kuzifikia baa nyingi zaidi na wateja wengi zaidi ambapo pia tunatoa zawadi nyingi zaidi kwa wateja wetu tukiwashukuru na kusema asante kwa kuwa pamoja na bia ya Tusker muda wote”.

Alisema tunafanya haya yote ili kuhakikisha kuwa tunaipa promosheni yetu ya Tusker Fanya Kweli Kiwanjani muonekano wa tofauti kidogo ili wateja wetu wazidi kuburudika na kuhamasika kutokana na ubunifu wetu”.

Aliongeza kuwa pamoja na kuwahamasisha watu kufikia malengo yao, sherehe hizi pia zinabeba ujumbe muhimu wa ubunifu katika kazi na jitihada katika maisha ili kuweza kuzifikia ndoto za maisha yetu.

Hii ni mara ya pili kwa promosheni hii ya Tusker kufanya sherehe za baa zilizo kwenye mkondo mmoja baada ya ile ya kwanza iliyofanyika Sinza Legho ambayo ilizikutanisha baa zaidi ya sita za eneo hilo zikiwemo:-Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.

Tusker Lager pia inayofuraha kuwapongeza washindi waliopo nje ya mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki katika promosheni hii ya Fanya Kweli Kiwanjani kwa wiki iliyopita, miongoni mwa baa hizo ni; - Geneva of Africa (Mrombo) na CR Pub (Moshono)-Arusha, Safari Pub ya Boma-Moshi, Cross Park (Igoma) na Kilimanjaro Pub (Nyegezi)-Mwanza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: