1. Jitume na ipende kazi unayoifanya
Ili ufanikiwe katika biashara yoyote, lazima uwe na moyo wa kujituma na uipende kazi unayoifanya. Usisubiri kusukumwa kwa sababu hakuna atakayefanya kazi hiyo. Jifunze kuwahi kuamka asubuhi ili uendane na kasi ya soko.

2. Kuwa na uwezo wa kuisimamia biashara yako
Wewe Kama Mjasiriamali ni lazima uwe na uwezo wa kuongoza na kusimamia biashara yako na kutoa maamuzi sahihi mara zote. Katika Ujasiriamali, uwezo wa kusimamia na kuwaongoza watu walio chini yako ni muhimu sana kwani hata kama ukianza na biashara ndogo, lazima baadaye itakuwa kubwa hivyo utalazimika kuajiri watu wengine wa kukusaidia.

3. Kuthubutu
Hapa nazungumzia uwezo na utayari wa kufanya uamuzi mgumu wa kuingia katika biashara au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara. Wengi wanaogopa kupata hasara, kuanguka mtaji au kufilisika. Mjasiriamali bora ni lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya mambo makubwa lakini uthubutu huo uendane na utafiti wa kina. Usiwekeze sehemu ambayo hujafanya utafiti wa kutosha.

4. Kuwa na Nidhamu
Nidhamu ni muhimu sana katika biashara, matumizi ya pesa, muda, nidhamu kwa wateja na kila kitu kinachohusu shughuli zako zinazokuingizia kipato. Nidhamu ni chanzo cha mafanikio kwani ndiyo inayosimamia sehemu kubwa ya biashara zako.

5. Kuwa makini
Wale waliofanikiwa siyo tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi walizokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa mwangalifu kwa kila jambo, anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe na uelewa wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko, uzalishaji na uendeshaji kwa jumla.

6. Kuwa mwaminifu
Uaminifu ni silaha kubwa itakayokulinda mjasiriamali na kuwafanya watu wengi wapende kufanya biashara na wewe.

Jifunze kulipa madeni hata kama ni madogo unapodaiwa, wauzie wateja wako huduma au bidhaa kwa bei halali,Kamwe usiwauzie watu bidhaa zilizokwisha muda wake, zenye ubora hafifu au mbovu kwani kwa kufanya hivyo, wateja watakukimbia na huo ndiyo utakuwa mwisho wa biashara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: