House girl alitandika kitanda cha bosi wake Kama Sehemu ya jukumu lake la kila siku. Alipomaliza akakitazama sana kile kitanda cha bosi wake akasema naweza kufa bure bila ya kulalia kitanda kama hiki. Akasema ngoja nijaribu kulala angalau kidogo.

Akavua nguo zote akaziweka chini, akabaki na gagulo tu akawasha AC akajifunika brangeti gubigubi akalala. Kwa bahati mbaya usingizi ukampitia kweli akalala fofofo.

Ghafla Mume wa bosi akarudi na haikuwa kawaida yake kurudi Muda huo. Alipoingia chumbani, akajua hakika huyu ni mke wangu na kwa kuwa jana tulikwaruzana atakuwa amekasirika tu. 

Akaogopa kumwamsha. Mwanamme akasaula, akabaki na msuli naye akajifunika hilo hilo blanketi kwa taratibu sana kwa hofu ya kumwamsha mke wake. Kwa bahati mbaya naye usingizi ukampitia, akalala fofofo.

Bosi aliporudi, akaingia chumbani, akakuta watu wawili wamelala fofofo. Akafunua blanketi kwa nguvu, akawakuta wote wawili; yaani yule mfanyakazi na mume wake wamelala pamoja. Walipoulizwa kila mtu akaeleza ukweli wake.

1. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule mke wa bosi ungewaelewa?

2. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule mfanyakazi ungejitetea vipi?

3. Je, Wewe ungekuwa ndiyo yule bosi ungejitetea vipi?

4. Je hapo ugomvi utakuwa umesababishwa nani? Mke, mume au mfanyakazi?

3. Story inawafunza nini mabosi, wake za mabosi na ma hausigeli?
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: