Waziri wa Uchukuzi na usafirishaji, Dr Harison Mwakembe akiongea machache katika uzinduzi wa Matairi maalum kwa mabasi (MICHELIN X COACH TROPIC Z).
Waziri wa Uchukuzi na usafirishaji, Dr Harison Mwakembe (c) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Matairi maalum kwa mabasi (MICHELIN X COACH TROPIC Z). kulia mwanzo ni Mkurugenzi wa masoko kanda ya Afrika Asia na Mashariki ya Kati kutoka kampuni ya Michelin Bw.Freddie Stoeffler anayefuata ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Super Doll na wauzaji wa matairi ya Michelin Tanzania, Bwana Seif Ally Seif, kushoto mwanzo ni Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra Gilliard Ngewe anayemfuatia ni Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Mohamed Ramadani Mpinga. Viongozi hao wamesema vifo vinavyo tokana na ajali ni vingi sana kwa hiyo. Wasafirishaji wanunue Matairi yenye ubora wa kimataifa ilikuokoa maisha ya Watanzania pamoja na fedha sherehe hiyo ya uzinduzi ilifanyika Makao Makuu ya Super Doll Tanzania na kuhudhuriwa na wamiliki wa mabasi hapa nchini. Picha na Chris Mfinanga.
Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji, Dr. Harison Mwakembe akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa mabasi ambao aliwatunukia vyeti kutokana na kununua kwa wingi matairi ya MICHELIN X COACH TROPIC Z kushoto ni mwakilishi kutoka kampuni ya usafishaji ya Abood Bus Mohhamed Abood na kulia ni mmiliki wa mabasi ya Dar Express, Bwana Mremi mwanzo kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Super Doll na wauzaji wa matairi ya Michelin Tanzania na kulia mwanzo ni Mkurugenzi wa Masoko Kanda ya Afrika Asia na Mashariki ya kati kutoka kampuni ya Michelin Bw. Freddie Stoeffler.
Viongozi hao wamesema vifo vinavyo tokana na ajali ni vingi sana kwa hiyo Wasafirishaji wanunue Matairi yenye ubora wa kimataifa ili kuokoa maisha ya Watanzania pamoja na fedha sherehe hiyo ya uzinduzi ilifanyika makao makuu ya Super Doll Tanzania na kuhudhuriwa na wamiliki wa mabasi hapa nchini. Picha na Chris Mfinanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: