Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga. Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.
Mhandisi Happiness Mgalula, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa barabara ya Tunduma – Sumbawanga . Mhandisi Mgalula anaongoza timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo  kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
 DSC 03923: Mhandisi Julius Isoka ambaye ni Mhandisi Mshauri wa Barabara ya Tunduma- Sumbawanga kutoka kampuni ya Nicholous Odweyer akiwaelezea timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao wanatembelea barabara hiyo jinsi ambavyo daraja linasukwa kutoka chini mpaka juu. Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa Marekani chini ya Mradi wa Milleniam Challenge (MCC).
Daraja la Kashahanzi moja ya daraja kubwa na linalojengwa kwa umahiri mkubwa katika barabara ya Tunduma –Sumbawanga.

PICHA ZOTE NA JOYCE MKINGA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: