Wadau wa Kundi la Kandanda katika Mtandao wa kijamii wa Facebook ambao leo wamekutana pamoja katika kusherehekea maadhimisho ya miaka minne ya Kundi hilo,kwa kusakata mtanange mkali sana katika Uwanja wa TCC Club,Changombe jijini Dar es Saalam.Mtanange huo ulizikutanisha timu mbili zilizoundwa na wadau Dizo Moja na Ismail.TeamDizo iliibuka kidedea kwa kuinyuka TeamIsmail mabao 4-1 bila huruma na kufanikiwa kutwaa kombe la shampeni.
 Muanzilishi wa Kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa kijamii wa Facebook, Patrick Dumulinyi (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ubingwa kwa Nahodha wa TeamDizomoja,Husolin Ulomi baada ya kuishinda TeamIsmail mabao 4-1 katika mtanange wa kuadhimisha miaka minne ya kuanzishwa kwa kundi hilo,leo kwenye Uwanja wa TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
 Muanzilishi wa Kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa kijamii wa Facebook,Patrick Dumulinyi. 
 Mwali katulia kusubiri kwa kwenda wakati wa mtanage huo.
 Beki wa TeamIsmail akichambuliwa na Beki wa TeamDizomoja wakati wa mchezo wa kuadhimisha miaka minne ya kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa Facebook,uliochezwa asubuhi ya leo kwenye Uwanja wa TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa TeamIsmail,Majaliwa Mkinga (kushoto) akionyesha ufundi wake mbele ya Beki wa TeamDizomoja katika mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa TCC,Chang'ombe jijini Dar.hadi mwisho wa Mchezo TeamDizomoja iliibuka kidedea kwa ushindi Mnono wa Mabao 4-1.
Super Sub wa TeamIsmail,Nassor Binslum akimtoka mchezaji wa TeamDizomoja,Damas.
 Hatariiii pale langoni kwa TeamDizomoja.......
 Benchi la Ufundi la TeamDizomoja.
 Benchi la Ufundi la TeamIsmail.
 Mwali na zawadi.
 Straika wa kutumainiwa wa TeamDizomo aliegusa mpira mara mbili tu kwa dakika 90 za mchezo,Balozi Kindamba akionyesha mambo yake
 Makocha waandamizi wa TeamDizomoja na TeamIsmail wakifatilia mchezo kwa umakini.
 Kiungo wa TeamIsmail,Vicent Ngailo akifanya yake mbele ya beki wa TeamDizomoja
 Anacheza vyema kabisa nyanda wa TeamDizomoja.
 haya twendeeeee.....
 Mshambuliaji machachari wa TeamDizomoja aliepachika mabao matatu peke yake,SillaYalonde akiondoka na mpira kuelekea langoni mwa timu pinzani.
Kocha mchezaji wa TeamDizomoja,Dizomoja akimpiga utajiju moja Beki wa TeamIsmail katika mtanange wa nguvu uliopigwa leo kwenye uwanja wa TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
 Anapiga tiktak maridadi lakini inakwenda njeee....
 Wawili kwa mmoja.harariiiii. Picha zote na Othman Michuzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: