Mtalaam wa Mawasiliano wa Tigo Amani Nkurlu (kulia) akikabidhi tuzo ya 'Tigo Best Short Film' kwa Mtayarishaji wa Filamu kutoka Kenya Mark Maina katika Maonesho ya Filamu ya Kiafrika Arusha (AAFF) aliyeshinda kupitia filamu yake mpya iitwayo "Consigned to Oblivion." Maonesho hayo yaliyodhaminiwa na Tigo yalifikia tamati juzi.
Mratibu wa maonesho ya AAFF Nassir Mohamed akionyesha tuzo aliyoipokea kwa niaba ya Muongozaji filamu kutoka Tanzania Amil Shivji aliyeshinda tuzo ya 'Best Short Film' kwa ukanda wa Afrika Mashariki kupitia filamu yake mpya iitwayo "Samaki Mchangani." Akishuhudia kulia ni Mtalaam wa Mawasiliano wa Tigo Amani Nkurlu.
Wacheza filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki (Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Tanzania na Zanzibar) wakionesha vyeti vyao ya kuhitimu mafunzo maalum ya uchezaji na uandaaji wa filamu kutoka wagwiji mbali mbali wa uandaaji wa filamu barani Afrika.
Wageni waalikwa mbali mbali na wapenzi wa filamu wakipata burudani kutoka kundi la Reggae kutoka Tanzania, Kenya na Marekani 'The Warriors from the East' wakitoa burudani
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: