Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jana usiku Oktoba 9, 2014 jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile, Freddie Manento, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi wa Uzazi Uzima, Dkt. Benatus Sambili (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akielezeewa kuhusu miradi inayosimamiwa na Amref Afrika, katika hafla ya Chakula cha Hisani kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Kujenga Uwezo katika mradi wa Uzazi Uzima wa Amref, Dkt. Pius Chaya (kushoto) wakati alipokuwa akielezeewa kuhusu miradi inayosimamiwa na Amref Afrika, katika hafla ya Chakula cha Hisani kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika, Dkt. Festus Ilako. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: